bwana na bibi ndo yeye
Mwanamke mmoja wa nchini Marekani ametoa kali ya mwaka kwa kuamua kuandaa harusi na kujioa yeye mwenyewe kanisani.
Nadine Schweigert mwenye umri wa miaka 36 amekuwa gumzo kwenye vyombo vya habari nchini Marekani baada ya kuandaa harusi na kujioa yeye mwenyewe ambapo yeye ndiye alikuwa bi harusi na yeye pia ndiye aliyekuwa bwana harusi.Nadine ambaye ni mkazi wa Fargo, North Dakota nchini Marekani alijioa mwenyewe kwenye sherehe iliyohudhuriwa na jumla ya watu 40.
Alikula viapo vya ndoa mbele ya umati huo wa watu ambapo mwisho wa viapo alipuliza busu angani badala ya hali iliyozoeleka ya bibi na bwana harusi kubusiana.Harusi hiyo ilifuatiliwa na fungate la nguvu (honeymoon) kwenye hoteli moja mjini New Orleans.
Akiielezea ndoa yake hiyo kwenye kipindi cha televisheni moja nchini humo, Nadine alisema kuwa hivi sasa anajihisi ni mwenye furaha sana na ndoa yake imeweza kuyabadilisha maisha yake toka kwenye huzuni na kuwa mwenye furaha sana.
Nadine alisema kuwa aliamua kujioa mwenyewe baada ya ndoa yake na mumewe aliyezaa naye watoto wawili ilipovunjika na watoto wake kuamua kwenda kuishi na baba yao.
Nadine alisema kuwa alipita kipindi kigumu sana cha machungu ya kuvunjika kwa ndoa yake lakini baadae aliamua kukaa chini na kutafakari maisha yake badala ya kujiingiza kwenye ulevi ili kupoteza mawazo.
Nadine aliongeza kuwa ndipo alipogundua kuwa furaha ya kweli na mtu anayempenda sana ni yeye mwenyewe hivyo akaamua kujioa yeye mwenyewe na hivi sasa haitaji tena mwanaume kwenye maisha yake.Nadine aliongeza kuwa katika maisha yake haya mapya amekuwa akijitoa out mara kwa mara na amekuwa akijinunulia zawadi yeye mwenyewe.
No comments:
Post a Comment