Robin Gibbs enzi za uhai wake.
Gwiji la muziki nchini Uingereza Robin Gibbs ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 62.Gibbs ni muasisina muanzilishi wa bendi hiyo maarufu ya Bee Gees na alikua akisumbuliwa na maradhi ya kansa na upasuaji wa tumbo.Gibbs ambaye ni mzaliwa wa nchini Uingereza alianza sanaa ya muziki alipounda kundi bendi ya Bee Gees akiwa na kaka zake wawili Barry na Maurice mnamo mwaka 1958.
Bendi ya Bee Gees ni bendi iliyokua ikivuma na maarufu sana na ilikua ikiuza rekodi zake nyingi sana kwa zaidi ya miaka 50 zikiwemo Stayin Alive, How deep is Your love, Massachusetts na Night Fever.Bee Gees walioa album amabazo zilikua zikiwaingizia mauzo ya mamilioni ya dola kote duniani tangu kuanza kwa bendi hiyo na kuwafanya namba moja.
No comments:
Post a Comment