utamtaka! hahahhh
Hebu tumtazame kwa Muktasari Dikteta Mobutu
Cheo ni kileo kibaya sana endapo utashindwa kuki control! Ukiachiia sifa ikuvae na usitende haki wewe kwishney! Mobutu kwa tabia!alipenda sana Wakongo wamuimbe yeye. Wampigie makofi hata kwa kauli za kipumbavu. Alishindwa kuelewa, kuwa unaweza kumpeleka punda mtoni, lakini kamwe huwezi kumlazimisha kuyanywa maji. Kwamba unaweza kumlazimisha mwanadamu kukupigia makofi, lakini kamwe si kutabasamu. Hilo la mwisho hutoka moyoni.
Mobutu hakuheshimiwa na watu wake, aliogopwa. Na sifa moja ya madikteta ni kuogopwa. Mobutu hakujishugughulisha na chochote kinachoitwa ujenzi wa taifa. Kinyume chake, alijaribu kuligawa taifa katika makundi kadri alivyoweza. Aliamini, kuwa kwa namna hiyo ndivyo angeweza kuwatawala vema Wakongo.
Kwa asili Mobutu alitoka kijiji cha Badolite, huko alijenga Ikulu ya marumaru za dhahabu. Ikulu ya Badolite ilikuwa ni kama mji wa kisasa wenye kila kitu. Ilikuwa ni Ikulu ya kifahari kweli. Lakini, ukitoka kilomita chache tu nje ya Ikulu hiyo, ulikutana na Wakongo walioshi katika umasikini wa kutupwa.
Katika mwaka wa mwisho wa utawala wa Mobutu, wananchi masikini walioishi kandokando ya Ikulu ya Badolite walikuwa na mazoea ya kuusimamisha msafara wa Mobutu. Naye Mobutu alifahamu, kuwa angesimamishwa, alichofanya Mobutu ni kuwaelekeza Wakongo wale waende kwenye gari la nyuma kwenye msafara wake. Huko kulikuwa na wapambe wa Mobutu waliokuwa na maboksi ya fedha za Kikongo, walizigawa. Wakongo wale walibaki wakizigombania, msafara wa Mobutu uliendelea.
Kitu ambacho Mobutu hakukitafakari ni ukweli, kuwa kugawa kwake noti zile kwa Wakongo hakukuwa jawabu la matatizo ya Wakongo. Watu wake walishawaganyika, na yeye Mobutu ndiye aliyechangia kuwagawa.
Mobutu aligawa utajiri wa rasilimali za Wakongo kwa wachache. Na yeye akawa mfano wa ufujaji wa rasilimali hizo. Tofauti na wakati wa mkombozi Patrick Lumumba, utaifa na moyo wa uzalendo uliporomoka kwa kasi ya ajabu miongoni mwa Wakongo.
Hatimaye, msafara wa mwisho wa Mobutu haukusimamishwa, kila mmoja alijua kuwa ulikuwa ni msafara wa mwisho kuelekea uwanja wa ndege kutoka Ikulu yake ya Kinshasa. Mobutu aliikimbia Zaire na kufia ughaibuni, kwenye nchi ya Morocco. Inasemekana, kuwa watu waliokwenda kumzika Mobutu hawakuzidi sita.

Viongozi Afrika wanapaswa kutambua sasa, kuwa Mwafrika wa mwaka 1975 si Mwafrika wa mwaka 2011. Waafrika wameamka. Viongozi Afrika wana lazima ya kuendana na mabadiliko ya wakati. Hizi ni zama za mabadiliko. Na Mabadiliko ya amani Afrika yanawezekana, mwenye kuyazuia mabadiliko ya amani, atambue, kuwa mabadiliko yenye vurugu hayaepukiki. Hilo la mwisho lina hasara kubwa. Mungu Ibariki Afrika na watu wake!.
Patrice Lumumba Patrice alikuwa mwanasiasa mwanamapinduzi wa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo . Mwaka wa 1958 alikuwa miongoni mwa waanzishaji wa Chama cha Taifa la Kongo . Mwaka wa 1960 alipata kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya kuongoza harakati za kugombea uhuru toka kwa utawala wa kikoloni wa Wabelgiji . Baada ya miezi miwili tu ya kuwa Waziri Mkuu, Lumumba alipinduliwa na baadaye kutiwa ndani kabla ya kuuawa katika mazingira ya kutatanisha katika eneo la Katanga upande wa kusini wa Kongo.
No comments:
Post a Comment