Thursday, May 17, 2012

Ukistaajabu ya Musa? Utayaona ya Firauni!




tumemsiki Rais Baraka Obama kuunga mkono ndoa za jinsia moja ,ulimwengu na viongozi wa dini wakamgeukia na shutuma kibao kua amewageuka na hakupaswa kuonesha msimamo wa namna hiyo, lakini unapostaajabu ya Musa utayaona ya Firaun, karibu katika ulimwengu wa ajabu wa ndoa ya mbwa wawili wa bi Ann Clark ,Mrs Clark ana umri wa miaka 55, aliyeamua kutoza paundi 150 sawa na laki 3 za Tanzania ili uweze kua mwalikwa wa sherehe ya mbwa wake, nan amekwisha ongoza sherehe kama saba hivi kwenye bustani yake  huko Northamptonshire, bibi huyo alikodi gari za gharama ,mapambo, wapiga picha mashuhuri  na mazagazaga mengine ili kuipamba sherehe hiyo iliyogharimu kiasi cha milioni 40 za Ki Tanzania kwa ajili ya marafiki zake hao wenye miguu minne. naomba ushuhudi mahaba haya ya mmiliki na mbwa wake.


                                           bwana na bi harusi wakiwa na mmiliki wao




          bi harusi akiandaliwa, gauni jeupe lenye neti kwa ndani ili lichanue ki sinderera

bibi huyu hakuishia hapo ameshawafungisha ndoa paka wawili, sungura nk ingawa dini haina nafasi katika hilo anachofanya ni kuvaa kola yake na kuwafungisha ndoa na baadae kutambua ndoa hiyo kwa tamko la na sasa ninyi ni bwana na bibi hahahaha hakiyanani wai ulimwengu huu? una mambo

kama mfanyavyo ninyi binadamu protokali huatwa hivyohivyo bwana harusi huingi pagoda na kwenda katikati ya bustani kumsubiri mtarajiwa,akishatoa tamko la kuwatambua basi picha za pamoja hupigwa kabla hawajaelekezwa kwenda kwenye sherehe ilikoandaliwa na mapochopocho hufuata,na  baada ya hapo bata ndeeefu huwa inafuata.


bibi  Betty White  mwenye miaka 90 naye!?  alimuachia mbwa  Uggie  ampe busu mdomoni! mh mi mahaba haya sina mwaya!


hahahahahahhahah mama mbavu zangu miye, baada ya kiss , mbwa huyo akaamua kuwafanyia mbwembwe wapigapicha , hebu ona mwe! mwe! mwe!


hahahaha kweli hii ndio dunia! Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firaun.

No comments:

Post a Comment