ZANTEL YAZINDUA OFA MBILI MPYA- UHURU KWA TANZANIA BARA NA UMOJA KWA TANZANIA VISIWANI
Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel Zanzibar Mohammed Mussa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na viwango vya Umoja ambavyo vinawawezesha wateja wetu walio visiwa vya Zanzibar kuongea kwa robo shilingi kuanzia saa nne usiku hadi saa moja asubuhi. Pembeni mwake ni Afisa Mkuu Biashara wa Zantel Ahmed Mokhles.
|
Afisa Mkuu Biashara wa Zantel Ahmed Mokhles (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wakati wa uzinduzi wa ofa ya Isiyo na Kifani inayowawezesha wateja wa Zantel kupiga simu kwa nusu shilingi kwa masaa 24 na kwenda mitandao mingine kwa TSH 2 kwa sekunde siku nzima. Kulia ni Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel Zanzibar Mohammed Mussa na aliyeketi kushoto ni Chief Mwakibete Mkurugenzi wa Bigtone LTD wakala mkuu wa Zantel.
|
Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel, imezindua ofa mbili mpya za kipekee kwa wateja wake wa Tanzania bara na visiwani zitakazoifanya kuwa mtandao nafuu zaidi nchini. Wateja wa Zantel Bara watafaidika na ofa ya UHURU ambayo itawawezesha kupiga simu kwa nusu shilingi (0.5) kwa sekunde muda wote. Ofa hii ya Uhuru itawawezesha pia kupiga mitandao yote nchini kwa shilingi 2 tu kwa sekunde. Zaidi ya hayo, ofa ya Uhuru itamuwezesha mteja kupiga kwenda nchi tano (Kenya, India, Pakistan, UAE and China) kwa shilingi 4 tu kwa sekunde siku nzima.
Wakati huo huo, wateja wa Zantel Zanzibar watafaidika na ofa ya UMOJA ambayo itawawezesha kupiga simu kwa shilingi moja kwa sekunde saa 2 asubuhi hadi saa 11 jioni, na baada ya hapo kupiga kwa robo shilingi (0.25) kila baada ya dakika ya tatu ya maongezi. Ofa hii ya Umoja pia itawawezesha wateja wa Zantel Zanzibar kupiga mitandao yote kwa shilingi 2.50 kwa sekunde muda wote.
Kujiunga na ofa hizi, wateja wa Zantel wanatakiwa kupiga *148*06#, wakati wateja wapya wataunganishwa moja kwa moja wakiongeza muda wa maongezi wa shilingi 500, na moja kwa moja watapata meseji 1000 pamoja na mlio wa simu kwa kutumia mwezi mzima.
Akizungumzia ofa hizo, ya Uhuru na Umoja, Afsa masoko mkuu wa Zantel, Bwana Ahmed Mokhles anasema:
“Ofa hizi zote zinalenga kuwapa wateja wetu thamani ya pesa zao wakiwa wanawasiliana na ndugu zao, marafiki pamoja na wafanya biashara wenzao wakitumia mtandao wa Zantel.”
Katika kuonyesha pia Zantel ni mtandao unaowajali wateja wake, imeamua pia kuongeza muda wa promosheni yake ya TickTock na Ushinde baada ya kupata shuhuda toka kwa wateja wake namna ilivyoweza kuwasaidia kimaisha.
“Wakati baadhi wameweza kuwalipia ada ya shule watoto wao, wengine wameweza kufungua biashara zao wenyewe”anasema Bwana Mokhles.
Ticktock na ushinde ni promosheni ya kipekee iliyoanzishwa na Zantel kuanzia tarehe 1 mwezi wanne ambapo kila siku mshindi mmoja wa shilingi milioni moja na wengine 24 walikuwa wakijishindia simu za mkononi kila siku kwa kuongeza muda wa maongezi wa shilingi elfu moja au zaidi. “Tunafuraha kubwa kuongeza muda wa promosheni hii, ili tuwafikie wateja wengi Zaidi” anasisitiza Mokhles.
Sambamba na ofa hizo, Zantel pia itakuwa na ofa katika maduka yao na ofisi za huduma kwa wateja katika vituo vya Vuga, Chake Chake, Pemba na katika makao makuu ya Zantel , Dar es salaam, ambapo zawadi zaidi zitatolewa kwa wateja watakaoenda kuweka muda wa maongezi kupitia maduka ya Zantel au kupitia Mimina.
“Kwa shilingi 1,000 au zaidi wateja wetu wana nafasi ya kushinda zawadi za papo kwa papo kama miavuli, peni, tisheti na nyingine nyingi” anasema mkurugenzi wa Masoko wa Zantel-Zanzibar Bwana Mohamed Mussa.
Huduma hizi zote ni sehemu ya ahadi za Zantel kuwa kampuni ya simu inayompa mteja wake huduma bora kwa gharama nafuu kabisa.
-kila lakheri wateja wa Zantel katika kuzitumia ofa hizo mbili za kipekee
No comments:
Post a Comment