Shirika la Save the Children katika taarifa yake limesema hali huko Niger inazidi kuwa mbaya zaidi.Shirika hilo linasema kuwa watu zaidi ya milioni sita wanakabiliwa na njaa. Na katika eneo zima la Sahel karibu watu milioni 18 wanakabiliwa na tishio la njaa.
Taarifa hiyo inasema kuwa idadi ya watoto wanaohitaji matibabu kutoka na maradhi yanayotokana na ukosefu wa chakula imefikia kiwango cha kutisha.Onyo hilo la Save the Children linakuja wakati mataifa tajiri zaidi duniani G8 yanakutana kujadili hali ya chakula duniani.
Shirika hilo linasema kuwa kwa wakati huu wanafanya mipango ya dharura kukabiliana na hali hiyo.Tangu mwaka jana wakati mvua ya masika iliyotarajiwa haikunyesha vizuri jamii ya kimataifa ilianza kutoa ilani kuwa hali huenda ikawa mbaya katika eneo la Sahel na hasa Niger.
Kijumla asilimia 25 ya watoto wote duniani wanakabiliwa na matatizo ya utapiamlo. Wengi wa watoto hao wako bara la Afrika.Sasa shirika la Save the Children limeomba vingozi wa nchi za G8 wanaokutana Marekani washughulikie hali hiyo.
No comments:
Post a Comment