Friday, May 4, 2012

Mauaji ya Mwandishi

                                                      Wanamgambo wa Somalia


Huku ulimwengi ukiadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari hapo jana, mwandishi mmoja wa habari wa kituo cha redio cha Daljir, nchini Somalia, ameuwawa kwa kupigwa risasi na watu walio kuwa wamejihami kwa silaha kali mjini Galkayo Kaskazini mwa nchi ya Somalia .
Hilo ni tukio la tano la mauaji ya aina hiyo kufanyika  kwa mwaka huu.
Mwandishi wenzake wa habari wa kituo hicho cha redio, Farhan Jeemis Abdulle, amesema kuwa wakati akitoka ofisini, walifyatuliwa risasi na watu waliokuwa wameficha nyuso zao.
Shirika la Uhuru wa Vyombo vya Habari la Reporters Without Borders, limesema Somalia ni nchi hatari kuliko zote kwa mtu kufanyakazi ya uandishi wa habari.
Zaidi ya waandishi wa habari 30 wameuawa katika kipindi cha miaka 5 iliyopita Somalia

No comments:

Post a Comment