Wednesday, May 2, 2012

Mapigano yaendelea kwa siku ya pili

Mapigano yaendelea kwa siku ya pili

Jeshi la Mali
Jeshi la Mali
Wanajeshi waliompindua rais was Mali aliyeondoka mamlakani, Amadou Toumani Toure, wametangaza kuwa wamedhibiti kambi kuu ya kijeshi katika mji mkuu wa Mali, Bamako.
Tangazo hilo limetolea baada ya makabiliano na wanajeshi waliotaka kumrejesha mamlakani kiongozi huyo wa zamani.
Wanajeshi hao ambao hadi sasa wangali wanadumisha amani mjini Bamako, walikabiliana na mahasimu wao wanaodai wanataka kumrejesha mamlakani Bwana Toure, kwa siku mbili mfululizo.

Risasi zasikika

Makabiliano ya risasi yalianza kusikika mjini Bamako Jumatatu Alasiri baada ya ripoti kutokea kuwa kulikuwa na mipango ya kuwatia mbaroni walinzi wa Rais huyo wa zamani.
Jeshi lilimpindua Rais Amadou Toumani Toure, Machi lakini likaondoka madarakani majuma matatu baadaye.
Hata hivyo jeshi lina ushawishi mkubwa kwa sababu bado lina viti vitatu katika Baraza la Mawaziri.
Mkurugenzi wa Hospitali kuu ya Gabriel Toure, Abdoulare Nene Coulibaly, aliwaambia waandishi wa habari kuwa watu 14 waliuawa katika mapigano hayo ya siku mbili.

No comments:

Post a Comment