Tangu rais wa Marekani Barack Obama alipofunguka hadharani kua anawatambua wapenzi na ndoa za jinsia moja! wiki moja iliyopita kuna mjadala mkali unaondele duniani ikiwemo nchi yake ya Kenya kumuona kama msaliti kwa kuunga mkono mapenzi ya jinsia moja ,wakati ulimwengu ukimshambulia Rais Obama kwa msimamo wake huo! baba Jayz a.k.a baba Ivy star mwenye nguvu na ushawishi nchini Marekani yeye ameweka kando lawama hizo na kuamua bila hofu kumuunga mkono raisi wake
na hilo limetokea wakati Jayz alipokua kwenye press Conference na waandishi wa habari huko Philadelphia kuwaeleza juu ya music festival yake atakayo ifanya mwezi September, lakini pia star huyo aliongea na CCN juu ya uamuzi wa Rais Obama na hapa namnukuu kwamba muda wote amekua akilifikiria suala hilo kua linairudisha nchi ya Marekani nyuma,watu wanachokifanya majumbani mwao ni matakwa yao na unaweza kumchagua mpenzi umpendae ili muwe katika mahusiano, na kulipinga hilo halina tofauti na ubaguzi wa rangi kwa watu weusi,ni ubaguzi wa wazi. Jayz anasema ni kitu kizuri hata kama raia hawatampigia kura na hilo halihusiani na uchaguzi .
kutokana na kauli na msimamo wa Rais Obama vikundi mbali mbali vya kidini vimefadhaishwa sana na uamuzi wake.
Jay, ambaye amekaa kwenye chati top 5 ya ma rapper ambao wamo kwenye hip hop na wanakamata nmkwanja mrefu kwa muujibu wa Forbes Magazine ,Jay ameungana na wasanii wenzake mashuhuri kama Mariah Carey, Russell Simmons na Janet Jackson ambao msimamo wao ni kutetea mapenzi ya jinsia moja na wanaunga mkono ndoa za mashoga .
No comments:
Post a Comment