Friday, May 4, 2012

Naibu Spika Atupa Vidonge Vyombo Vya Habari

                                                        Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai

Naibu spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, amevitaka vyombo vya habari nchini kutoa habari zinazozingatia pande mbili za shilingi ili kutoa nafasi kwa wote wanaozungumziwa kupata nafasi ya kujieleza.
naibu spika ameeleza kua kuandikwa kwa habari zisizokua na upendeleo kwa upande fulani kutasaidia wananchi  kuelewa ukweli kuhusu kinachoandikwa au kutangazwa na kushauri kua serikali isikosolewe peke yake bali na pande nyingine zisizokua madarakani zikosolewe ili zikishika madaraka zitekeleze wajibu wake ipasavyo.
amesema Vyombo vya Habari nchini vinatakiwa kutumia uhuru wake kwa kurekebisha makosa yaliyopo katika idara,taasisi za uuma na mashirika binafsi pamoja na serikali kwa ujumla bila kuegemea upande wowote.
kazi kwenu waandishi na vyombo vya habari.

No comments:

Post a Comment