Showing posts with label Urembo. Show all posts
Showing posts with label Urembo. Show all posts

Tuesday, December 17, 2013

WANAUME MTAUA WANAWAKE! YOTE HII NI KWAA AJILI YENU!




Sasa wanawake wapendao urembo na kuongeza mvuto wa mapenzi wanakwenda mbali, nasema hivi kwasababu, wapo walotoboa kila sehemu yam iili yao na kuweka kitu cha kipekee ili kuongeza mvuto wa kimapenzi badala ya kwenda kwa mganga!

Monday, November 25, 2013

MISS ILALA 2013 DORICE MOLLEL HANDS OVER 132 STORY BOOKS WORTH 200,000 TO UKONGA PRIMARY SCHOOL


Mkuki wa Nyota Editor Godance Mkuki(right) hands over 132 story books to Miss Ilala 2013 Doris Mollel at the Ukonga primary school premises in Dar es Salaam during the climax celebration of the International Children’s day.

Wednesday, June 5, 2013

LUNDENGA: MASHINDANO YA MISS TANZANIA HAKUNA RUSHWA YA NGONO

 Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga, akizungumza na warembo wanaotarajia kushiriki shindano la Redd's Miss Tanzania, 2013 wakati alipowatembelea kwenye kambi yao ya mazoezi yanayoendelea katika Ukumbi wa Meeda Pub. Shindano hilo linatarajia kufanyika Juni 7 mwaka huu katika ukumbi huo huo.

Monday, June 3, 2013

MISS DAR CITY CENTER YAKAMILIKA

  kati kati iss Dar city centre 2013,Alice Isack akiwa na mshindi wa pili, Clarah Paul (kulia) na mshindi wa tatu, Fatma Hussein (kushoto)

Thursday, May 30, 2013

BRIGIT ALFRED AWAFUNDA WAREMBO WA REDD'S MISS SINZA 2013


 Miss Sinza na Miss Tanzania 2012-2013, Brigit Alfred (kulia) akizungumza na Warembo wanaotarajia kuwania Taji la Redd's Miss Sinza 2013, wakati alipowatembelea katika Kambi yao ya mazoezi jana katika Ukumbi wa Meeda Sinza na kuwafunda kuhusu mashindano hayo kuelekea shindano hilo linalotarajia kufanyika Juni 7,mwaka huu kwenye Ukumbi huo. Katika shindano hilo Viingilio vitakuwa ni Sh. 20,000 kwa VIP na viti vya kawaida ni Sh. 10,000. Shindano hilo limedhaminiwa na Mtandao wa www.sufianimafoto.com, kinywaji cha Dodoma Wine, Chilly Willy Energy Drink, Clouds Media Group, CXC Africa, Saluti5 na Fredito Entertainment.

Thursday, March 14, 2013

Wednesday, February 20, 2013

Hair dyes used by millions of women are linked to chemicals that can cause cancer





 High risk beauty: The hair dye chemicals could react with tobacco smoke and exhaust fumes, to form highly poisonous chemicals called N-nitrosamines



Hair dyes used by millions of women contain chemicals linked to cancer, British scientists have warned.
They say that both home hair colouring kits and the dyes used at expensive salons pose a potential risk to health.

Monday, December 17, 2012

SERIKAKALI YABARIKI MAANDALIZI YA FAINALI ZA MISS UTALII TANZANIA 2012/2013


VIONGOZI WA BARAZA LA SANAA LA TAIFA (BASATA) WAKIWA KATIKA MKUTANO WA  MAANDALIZI YA FAINALI ZA TAIFA ZA MISS UTALII TANZANIA  NA BODI  YA MISS UTALII TANZANIA 2012/2013 ZITAKAZO FANYIKA HIVI KARIBUNI.

Friday, September 28, 2012

The Rise And Rise Of Matata Fahari ya Tanzania!!!

Flaviana Matata (© Facebook) 


Africa ni sehemu pekee ambako ma models hukuzwa kuanzia level ya chini hadi kufikia kiwango cha juu, nah ii ni kwa miaka mingi iliyopita na kufanikiwa kuchangia ukuaji wa biashara models.
katika miaka ya hivi karibuni, maonesho kadhaa ya mavazi ambayo huendeshwa nje na ndani ya bara la Afrika basi hukosi kuwashuhudia models wa bara kubwa Africa!
 
Flaviana Matata (© Facebook) 


Model Flaviana Matata,  kutoka nyumbani Tanzania ana umri wa miaka 25 , na anajulikana kimataifa kwa kazi zake zilizotukuka za modeling  na kujinyakulia sifa ya becoming one of the world’s brightest stars.

Friday, May 25, 2012

Picha za Siku ya Leo


Mungu kweli anaumba! kindege kinatabasamu hadi kimefumba macho, halafu Mungu akampamba kwa hiyo rangi juu ya macho yake sijui niseme nyusi? kazurije? wow asante Mungu kwa uumbaji.



wako katika mazoezi ya yoga, Mungu ni waajabu sana wanyama wakifundishwa kwa Lugha zetu wanaelewa na kufuata maelekezo yote uwapayo.mbwa ni rafiki muaminifu na mlinzi mzuri sana mi huwa napenda aina ya mbwa kama wale wa feed Force.






Picha ya Leo


hii ni picha ya leo nimependa alivyopambwa! zaidi sana kicheko chake ndege huyu!

Tuesday, May 22, 2012

Maonesho ya sanaa Ivory Coast



kama ujuavyo katika vyombo vya usafiri kuna mengi, sogea huko mtu hataki, akibanwa analalamika ,alalamikapo hupewa neno kua kama anaona anabanwa  basi akapande taxi,na mengi mengineyo.lakini ndani ya daladala  vibweka na vibwakuro ni sehemu ya maisha ya kila siku katika usafiri huo wa jamii.
huko mjini Abidjan konda aliamua kumfokea mwanamke mnene kua anachukua nafasi kubwa ya watu wawili anakaa yeye mwenyewe, hivyo kama anataka apande! basi alipe nauli ya watu wawili,anasimulia mchoraji wa picha hiyo hapo juu aitwae Augustin  Kassi.
baadhi ya tamaduni hapa ulimwenguni hususani Ghana na Ivory Coast  wanawaheshimu sana wanawake wanene kwani wanatoa ishara kwamba waume zao wanawatunza vyema na miili yao imeonesha shukrani  tena akiisha pata mtoto waume hushughulika kulisha vyema wake zao ili watokapo kwenye arobaini baada ya kujifungua basi wawe wamebadili , hili limeenea sana Mkoani Kilimanjaro na mtazamo kama huo wa kupenda wanwake wanenen kwa hapa Kwetu Tanzania uko mkoa wa Mbeya.


wachoraji wa mambo ya maumbile, wanajivunia sana kuchora marembo ya dunia ikiwemo maua, mimea,wanyama, na wanaona fahari kuona viumbe vyote vinaishi kwa amani.maonesho hayo yamefanyika mwezi huu wote huko Abidjan Ivory Coast ambayo yalihusisha michoro ya kipekee ni   wanawake wenye maumbile manene,Augustin Kassi  ambaye ni mchoraji mashuhuri nchini Ivory Coast  akiwa na nia ya kubadilisha dhana ya kuwadharau wanwake wanene ambao mara kwa mara wanachekwa kutokana na taswira yao, na yeye ameamua kundaa maonesho hayo kwa kumuiga roll model wake mchoraji kutoka nchini Uingereza  Beryl Cook .




Kassi anasema muhimu ni kuwapa moyo wanawake wanene badala ya kuwacheka na kuwadharau.




Augutine Kassi- mchoraji na mwanaharakati wa kutetea wanawake wanene, hahahahha

Thursday, May 17, 2012

Nguvu ya Vitu Vya Asili Katika Ngozi Yako

kama wewe unapenda urembo  na unaijali ngozi yako basi unaweza kutumia vitu vya asili badala ya vile vyenye madhara ambavyo vinaweza kudhuru ngozi yako .na vitu vya asili unavyoweza kutumia ni  kama mayai,mdalasini na asali huweza kukupa mn'garo mzuri lakini zaidi sana kwa wale wanaoupinga uzee mchanganyiko huo huweza kunyanyua uso wako na kuondoa mikunjo. wenyewe wanaita face lift. hebu nikupe vitendea kazi na mwisho nikupe namna ya kufanya.

                                                                           Asali

                                                               mdalasini




                                                                     Mayai

sasa! unachotakiwa kufanya ni hivi, unachukua ute wa mayai,maji ya limao ama ndimu kijiko kidogo, unga wa mdalasini kijiko kidogo,sukari kiasi na mafuta ya olive oil kijikom kidogo. changanya  pamoja na baada ya kuchanganya pakaa kwenye viwiko vya mikono, unaweza kupakaa midomo yao na usoni kwa ujumla kaa nayo mpaka itakauka, usisugue ondoa kwa kitambaa laini chenye maji ya baridi ,ukisha ondoa yote vizuri unaweza kunawa vizuri kwa maji safi na utakua tayari endapo utahitaji kutoka ama kupaka make up. jaribu uone , dada Lisa Rinna hapa chini ni shuhuda wa mchanganyo huo.



                                                                    Lisa Rinna

Saturday, May 12, 2012

Siku Ya Mapumziko na Usafi






 Leo ni siku ya mapumziko kwa walio wengi na wachache huenda kazini kama kawaida japo iwe nusu siku! nataka niwaangalie wanawake wafanya kazi walioko katika miji mikubwa! wao kwao leo ni siku ya usafi wa miili yao.kucha na miguu kusuguliwa! hilo halina tatizo! mi nachoshwa na huu urembo wa nyongeza. kope, tatoo, na midomo!
huwa tuna sema kazi ya mola haina makosa! sasa iweje watu waikosoe kazi ya Mungu? kwa kuongeza vitu? hii ina maana gani? na kwa faida ya nani? kama wewe mzuri mzuri tu! mnisamehe maana namimi pengine mshamba! ila madhara yapo! mkubali ama mkatae habari ndo hiyo! tuanze na kope


                                                              kope za wenyewe lol
siwasemi mnaoziweka hapana! najaribu kuwaza kwa sauti tu! kwa raha zenu? ama kwa faida ya nani? ninao marafiki wanao ziweka hizo ila sina jibu la moja kwa moja. nlipotaka kubandika, nikaogopa kutokana na rafiki zangu wawili waliwahi kuweka wakaumia! sasa sijui muwekaji fake? au gundi ndo feki? nikaona isiwe taabu.


        
                                                                nyusi za tatoo

sijui ni kutokua na muda?au ninini wanawake wameamua kunyoa nyusi zote na kubaki kipara na kisha mashine ama sindano kupita juu ya nyusi  zao na kuchora mchoro usio toka milele! next time ntakuletea tatoo za wanaume na mvuto wake.

kama hiyo haitoshi wanawake naona wamechoka kupaka paka lipstick zinazotoka basi wameamua kuchora midomo tatoo za rangi mdomoni kuepusha usumbufu ,ila najiuliza je ukienda msibana na tatoo ya rangi ya mdomo na nyusi zimechorwaa? waswahili watakufikiriaje? najua watoto wa mjini hawajali na misiba sasa hivi sio kiviile kama zamani.

                             huu mdomo ndo ushachorwa kazi kubwa ni lipbam au lipshine!



                                                        umeona bana! inapendeza kiukweli






            mrembo amechonga nyuzi zake na kope zake za asili saafi kapendeza!     maashallah        






                    
                                 wino unaohusika midomoni  na mwilini hiyo ni red kala! lol

well pendezeni wanawake wenzangu, hiyo huongeza confidance kiukweli! jumamosi njema.


Monday, April 30, 2012

Jicho Limekubalije?

Kiukweli kabisa! si kila mtu anayeiweza hii sanaa ya jicho! kuchonga nyusi iendane na jicho la mhusika! si wote! wengi  huwa wanaharibu muonekano wa jicho la mtu!

kutoka ndani ya nafsi yangu ningetamani mi kuwa na uwezo wa kumchonga mtu nyusi akapendeza kama huyu ,ingawa huwa nawachonga baadhi ya watu ambao huwa wanaamini nawapatia! lol

kope sasa! hilo jicho hapo juu limekubalije? hapo limefumbwa! likiinuliwa weee! utadhani anakwita kumbe anakutazama tu. eye shadow imekubali na kope zimebandikwa vizuri mnppp! hapo ndo nnapotamani kubandika ila nikifikiria gundi! mh naishiwa nguvu! big up kwa wale wanawapatia watu kuwapaka eye shadow ,kubandika kopa na kuchonga nyusi! ambao bado si vibaya kujifunza na kufanya vizuri zaidi!
jumatatu njema.