Hii ni moja kati ya
zile kesi za kanisa katoliki zilizodumu kwa muda mrefu kesi ilianza toka mwaka 2007 ambapo serikali ilitishia kulifungia gazeti la
kanisa katoliki endapo lingeendelea
kumuita Mungu Allah.
Taarifa ya sasa inasema
Mahakama kuu nchini Malaysia imetupilia mbali ombi la kanisa katoliki nchini
humo kumuita Mungu ‘Allah’ kwenye gazeti hili linaloandika habari zake kwa
lugha ya Ki malay.
Walidai kuwa Wakristo
wanawakanganya Waislamu walio wengi na hilo laweza kuhatarisha usalama wa taifa
ambapo uamuzi wa Mahakama ni mojawapo ya mikondo ya mwisho ya kesi za kisheria
za kanisa katoliki zilizochukua muda wa miaka saba na kusababisha mashambulizi
katika makanisa, majumba ya maombi ya waislamu na pia hekalu la wasikh mwaka
2010.
Shirika la habari la ulimwengu BBC wanaripoti kwamba Wakristo na wasikh wanadai kuwa
wamekuwa wakimwita Mungu ‘Allah’ katika lugha za kiMalay na Sansrit kwa muda
mrefu sana.
Mahakama nayo imeshikilia uamuzi wao wa awali kuwa jina hilo
halifai kuingizwa katika ukristo ambapo mgongano huu kuhusu neno hilo moja
umedhihirisha jinsi nchi hiyo yenye dini na kabila tofautitofauti
lilivyogawanyika.
Wanaharakati wa kiislamu wamekua wakishabikia uamuzi huo nje ya
Mahakama huku wengi wao wakiwa wanaamini kuwa wakristo wanamwita Mungu ‘Allah’
kama njia ya kuwavuta waislamu wajiunge na ukristo, shutma ambazo wakristo
wamekana.
No comments:
Post a Comment