Hatimaye Malawi imepata
Rais mpya baada ya mivutano ya kisheria kwa wiki nzima.
Mwandishi wa BBC Baruan
Muhuza amesema kutoka mjini Blantyre kuwa Profesa Peter Mutharika ameshinda
uchaguzi huo kwa kupata asilimia 36.4 ya kura zote akifuatiwa na Dr Lazarus
Chakwera mwenye asilimia 27.8 huku Rais anayemaliza muda wake Dr Joyce Banda
akishika nafasi ya tatu kwa asilimia 20.2 na Atupele Muluzi amekuwa wa nne na
asilimia 13.7
Mwenyekiti wa tume ya
uchaguzi Jaji Mackson Mbendera amesema uchaguzi huo ulikumbwa na changamoto
nyingi lakini mwishowe nchi ni lazima ipate kiongozi wake na kuwaomba wananchi
kuwa na utulivu .
KESI MAHAKAMANI
Awali Jaji Kenyata
Nyirenda wa mahakama kuu mjini humo jana usiku alitoa uamuzi kuwa hawezi
kuvunja sheria kwa kuruhusu tume iongeze muda wa kuhesabu upya kura kwenye
maeneo yenye utata.
Na kwamba sheria
inaitaka tume kutangaza matokeo ndani ya siku nane na si vinginevyo.
Uchaguzi wa Malawi
ulifanyika Mei 20 nchini kote lakini siku moja tu baada ya kupiga kura,
malalamiko yakiambatana na mapingamizi ya kisheria yakatawala kwenye mahakama
kuu za Lilongwe na Blantyre.
No comments:
Post a Comment