Showing posts with label AFYA. Show all posts
Showing posts with label AFYA. Show all posts

Wednesday, March 26, 2014

AFRICAN BARRICK GOLD MINING WADHAMINI TIBA YA UPASUAJI BURE KWA KICHWA, MGONGO NA MISHIPA YA FAHAMU KATIKA HOSPITALI YA BUGANDO MWANZA.

=
Daktari Bingwa wa Ubongo, Mgongo na mishipa ya fahamu Dr. Othman W. Kiloloma kutoka hospitali ya Muhimbili amesema kuwa timu ya madaktari saba imewasili kutoka Muhimbili  ikiwa na daktari bingwa 1 wa usingizi wakiwa na vifaa vyote muhimu ili kuungana na madaktari Bingwa wa upasuaji Bugando kwaajili ya kuweka kambi ya tiba mkoani Mwanza.

Thursday, March 7, 2013

MWENYEKITI WA JUKWAA LA WAHARIRI (ABSALOM KIBANDA) APELEKWA AFRIKA KUSINI KWA MATIBABU


Absalom Kibanda akiwa na mkewe ndani ya Ndege, Anjella Semaya, tayari kuanza safari ya kuelekea nchini Afrika ya Kusini kwa matibabu.

Wednesday, March 6, 2013

THE LETTER SENT BY GIRL, 11, WHO FEARED SHE BE CUT LIKE HER SISTER


Tunapoelekea kuadhimisha siku ya wanawake ulimwenguni! wapo watu ambao hata hawatamani kuisikia tarehe hiyo kila mwaka! kutokana na yanayo wasibu. ona hii , na huyu ni mmoja kati ya wengi ulimwenguni.utasoma barua yake chini inauma!


                                                Cry fo help

Wednesday, February 13, 2013

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr.Seif Rashid azindua huduma ya mawasilian​o bure kwa wahudumu wa Afya na madaktari nchini.


Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr.Seif Rashid(katikati),Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule (kulia) Mkurugenzi wa Shirika la Switchboard Ali Block wakionesha mabango ikiwa ni inshara ya uzinduzi wa kuwawezesha wahudumu wa Afya na madaktari kuwasiliana kwa simu za mkononi bure,huduma hiyo inatolewa na  Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Switchboard ili kurahisisha huduma za kiafya mahosipitalini.Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.

Friday, February 8, 2013

Wanaotumia runinga kwa muda mrefu hupoteza nguvu za kiume



AH HAHAHAHAHA KIJUKUUUUUUUUU! UNALO!
 WANAUME wanaotumia muda wa saa tatu na zaidi kwa siku kutazama runinga wanapoteza nguvu za kiume ukilinganisha na wale wanaotazama runinga mara chache.
Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Afya ya Umma cha Havard (HSPH) kilichopo Boston nchini Marekani, umebaini kuwa kuporomoka kwa kiwango cha mbegu za kiume kunahusiana moja kwa moja na kutofanya mazoezi na kutazama runinga kwa muda mrefu.

Monday, December 24, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATEMBELEA NA KUWAJULIA HALI WAZEE WA MKOKOTONI-MKOA WA KASKAZINI UNGUJA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mzee, Ali Mohamed Juma (85) Mkazi wa Mkokotoni Shangani Mkoa wa Kaskazini Unguja, wakati alipokuwa katika ziara yae ya kuwatembelea wazee kwa ajili ya kuwajulia hali, leo. Mzee huyo anasumbuliwa na ugonjwa wa kuvimba miguu .

Wednesday, December 12, 2012

RAIS KIKWETE APOKEA MAJENGO MAPYA MATATU YA HUDUMA ZA MAMA NA MTOTO DAR ES SALAAM



Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mbunge wa Ubungo Mhe John Mnyika na Balozi wa Korea kwa pamoja wakifungua rasmi jengo la Huduma za Mama na Mtoto katika Hospitali ya Sinza Palestine Kinondoni jijini Dar es salaam .
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mbunge wa Ubungo Mhe John Mnyika na Balozi wa Korea kwa pamoja wakifungua rasmi jengo la Huduma za Mama na Mtoto katika Hospitali ya Sinza Palestine Kinondoni jijini Dar es salaam .

Wednesday, November 21, 2012

RAIS JAKAYA KIKWETE AWAPONGEZA VODAFONE NA CCBRT




Rais Kikwwete akiongea wakati wa makabidhiano ya fedha za kusaidia kupambana na ugonjwa wa Fistula ,katika hospitali ya CCBRT jijini Dar-Es-Salaam,ambapo kampuni ya simu za kiganjani Vodacom Tanzania ,kupitia kampeni yake maalum iliyofanikishwa na huduma ya  Mpesa ,ilitoa kiasi cha pesa shilingi bilioni 8.
 

Thursday, November 15, 2012

MTOTO ALIYEUNGUZWA MKONO NA KULISHWA KINYESI AKATWA MKONO HOSPITALI YA RUFAA YA MBEYA




      

Hivi ndivyo anavyoonekana mtoto Aneth, alivyounguzwa na mama yake mdogo


                Sehemu ya uso ilivyo haribika.
 

huyu ndiyo mama mdogo wa aneth amejulikana kwa jina la  bahati lukangara ndiyo aliyemuunguza mtoto anethi.

Friday, November 9, 2012

KAMPENI YA UTOAJI HUDUMA KWA JAMII YAZINDULIWA


Chama cha madaktari wanawake Tanzania MEWATA jana kilizindua kampeni ya utoaji wa huduma mbalimbali za kiafya kwa jamii ikiwemo zoezi la uchunguzi wa saratani ya matiti,afya ya kinywa, saratani ya mlango wa uzazi,clinic kwa wanawake na watoto, upimaji wa macho  kwa wanawake katika mkoa wa Dar-Es-Salaam zoezi ambalo lilipata mwitikio mkuwa wa jamii kuchunguzwa afya zao.
Mgeni rasmi alikua mama Salma Kikwete First Lady, aliyewataka watanzania kuacha uvivu wa kucheck afya zao mara kwa mara.kushoto kwake ni Naibu Mwakilishi  wa mkuu wa mkoa  na kulia kwa mama ni Dr Sarafina Mkuwa mwenyekiti wa chama cha madaktari wanawake Tanzania a.k.a MEWATA.

Sunday, October 28, 2012

UGONJWA WA MARBUG UBAUA KWA ASILIMIA 70-90

Hapa ni nchini Uganda wataalamu wa Afya wakinyunyiza dawa mahali ambapo wagonjwa wa Marbug walitelekezwa hadi kufa, baada ya kugundulika wana ugonjwa huo.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII


 

 

 

 

TAARIFA KWA UMMA.

TAHADHARI YA UGONJWA WA MARBURG
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imepokea taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), tarehe 20 Oktoba, 2012 kuhusu ugonjwa wa Marburg ambao umejitokeza katika nchi jirani ya Uganda. Maeneo yaliyokumbwa na ugonjwa huo ni Wilaya ya Kabale, Kanda ya Kusini Magharibi ya nchi, na wilaya hii inapakana na Rwanda. Mpaka tarehe 24 Oktoba 2012, takriban watu 13 wamepata maambukizo na 6 wamepoteza maisha..