Daktari Feki
Hospitali ya taifa ya
Muhimbili imemkamata mtu mmoja anae sadikiwa kuwa daktari feki ambaye kwa
kipindi kirefu amekuwa akitapeli wagonjwa wanaoenda kutibiwa katika hospitali
hiyo ya taifa kwa namna mbalimbali
Daktari huyo aliyejulikana kwa jina la Kitano Mustafa Kitani mwenye umri miaka 51 anadaiwa kuwa alikuwa anajitambulisha kama daktari upande wa akina mama katika hospitali ya Muhimbili.
Hospitali ya taifa ya Muhimbili mbali na utaratibu wa kutumia vitambulisho kwa wafanyakazi ili kuondoa tatizo kama hili, bado tatizo hili limeendelea kujitokeza.
Hospitali ya Muhimbili inawataka wafanyakazi wake wanaoshirikiana na madaktari vishoka kuacha tabia hiyo yenye athari kwa wagonjwa na taifa.

CHAMA CHA MADAKTARI
Chama
cha Madaktari nchini kimewataka wananchi kuwa macho na madaktari
wanaojitokeza kutaka kusaidia wagonjwa.
Wakati daktari huyo akidai yeye ni daktari kitaaluma, Afisa Usalama hakubaliani nae kutokana na taarifa za kiuchunguzi kuthibitisha kuwa ni Daktari feki.
Wakati daktari huyo akidai yeye ni daktari kitaaluma, Afisa Usalama hakubaliani nae kutokana na taarifa za kiuchunguzi kuthibitisha kuwa ni Daktari feki.
NAMNA ALIVYONASWA
Eligaeshi alidai
maofisa usalama wa hospitali hiyo walipata taarifa za kuwapo kwa daktari
aliyeonekana akiwahudumia wagonjwa na kwenda kumkamata.
Baada ya kutiwa
mbaroni, inadaiwa alipekuliwa na kukutwa na kadi tatu za kliniki za wagonjwa wa
Muhimbili, kitambulisho cha Peter Daniel mfanyakazi wa hoteli moja Dar es
Salaam, vipimo vya kupimia ujauzito, namba nyingi za madaktari wa Muhimbili
kwenye simu yake ya mkononi na Sh167,000. Wakati akiwa chini ya ulinzi, mmoja
wa wagonjwa wake, aliyefahamika kwa jina la Hassan Madika alimpigia simu na
kutakiwa kwenda sehemu aliyokuwa akihojiwa. Mtuhumiwa alikiri kupigiwa simu na
Madika.
Daktari Feki Ajitetea
Kitano alisema kuwa
alifika hospitalini hapo baada ya Madika kumweleza kuwa alikuwa amefanyiwa
operesheni wiki iliyopita na kwamba, hawezi kusimama muda mrefu hivyo alikuwa
akihitaji msaada wa mtu wa kumpelekea faili sehemu husika.
Haji alipoulizwa na
waandishi wa habari, iwapo anamfahamu Kitano alisema alikiri kutomfahamu na
kwamba, hajawahi kumwona.
Alisema alifika
hospitalini hapo kumsaidi Madika na kwamba, tuhuma hizo zinalenga kumchafulia
jina hazina ukweli.
Hata hivyo, Kitano
alisema yeye siyo tapeli daktari na ameshafanya kazi hospitali mbalimbali za
Serikali.
Hili ni tukio la tatu
kutokea katika hospitali ya Muhimbili kwa Daktari Feki Kukamatwa.
No comments:
Post a Comment