Wandishi wa habari wakijadiliana juu ya tukio hilo huku wakiweka kumbukumbu kwa yale yanayopaswa kuwafikia walaji wa habari aka jamii. |
Kona ya wanahabari. |
Mkare Front Bar ni mmoja kati ya maeneo ya kiota hicho cha Skylight Beach Resort Mwanza, kitakacho tambulishwa ambapo Part hilo la Valentine linalo ambatana na tukio la Foolmoon Party litafanyika. |
This is Skylight Beach Resort. |
MWANZA.
KITUO kipya cha Burudani cha Skylight
Beach Resort, kilichopo Sweya Kata ya Mkolani Wilayani Nyamagana kuzinduliwa rasmi
siku ya Wapendanao (Valentines Day) kwa Tamasha kubwa la burudani ya ufukweni mwa
mwambao wa Ziwa Victoria Jijini hapa.
Kufunguliwa kwa kituo hiki ni moja kati
ya hatua za kuitikia wito wa serikali kwa wazalendo kuwekeza katika sekta ya
utalii na burudani kwenye maeneo
mbalimbali ya Majiji , Manispaa na Halmashauri za Wilaya.
Akizungumza na waandishi wa habari
Jijini humo jana, Mmoja wa Wakurugenzi wa Skylight beach Haruna Said alisema
kwamba, Kituo hicho kilichojengwa kwa hadhi ya Kimataifa na chenye madhari
nzuri ambacho kwa sasa ni gumzo na cha kwanza kwa ubora Jijini hapa.
Mkurugenzi huyo alieleza kuwa kabla ya
ufunguzi wa Ukumbi wa burudani wa Disko kuanza wamejipanga kuanza kutoa
burudani ya ufukweni maarufu Foolmoon Beach Part ambayo itakuwa inafanyika kila
mwezi mara moja kwa lengo la kutambulisha bidhaa mbalimbali zitakazopatikana
Skylight Beach Resort.
“Tumeazimia kuutangaza utamaduni mpya wa
Party kila mwezi kwa wakazi wa Jiji hili na wale wanaotoka maeneo ya Mikoa ya
jirani na nchi za jirani wanapofika kupata ladha mpya ya burudani ikizingatiwa
kituo hiki chenye hadhi ya kitalii kiko kilomita 10 kutoka Chuo Kikuu cha SAUT kilichopo
Malimbe Katani hapa”alisema
Aliongeza kuwa kufuatia siku hiyo
kuangukia siku ya wapendanao “Valentines Day”ambapo vilevile siku hiyo imeangukia
kwa tukio la mwezi kuonekana kikamilifu (Umbo la duara) klabu hiyo imenuia
kuwapa fursa watu wa burudani wa Jiji la Mwanza na wageni kusherehekea matukio
hayo kwa Tamasha la Skylight Fullmoon Party ikiwa ni juhudi za kukuza utalii na
uchumi.
“Moja ya bidhaa zitakazo nadiwa siku
hiyo ya Februari 14 mwaka huu kwa Watalii wa ndani na nje ambapo watapata fursa
maalumu ya wao kupata bidhaa ambazo ni vionjo
vipya vya Skylight Beach yaani Mamba Squre, Kiboko Tarrace na Mkare Front Bar
ambapo kwa watakaoingia watapata ladhaa na mitindo mipya kabisa” alisisitiza.
Naye Afisa Masoko wa Kampuni ya Syklight
Group Ltd, ‘Jembe ni Jembe’ alisema kuwa katika siku hii ya shangwe kwa wakazi
wa Rock city, kututakuwa na burudani mbalimbali toka kwa MAdj wakali, DVJ Frank,
DVJ Denis na DVJ Davy ambao watatambulisha mfumo mpya wa burudani ya
kiwango cha kimataifa. Pia tutakua na Dj mgeni (Guest DJ),kutoka Dar es salaam,
DVJ MAFUVU Atakayedondosha ngoma kali kwa watakao hudhuria.
.
“Tumejianda kutatoa zawadi kibao kwa
waliopendeza na kuvalia mavazi rasmi ya Valentine, huku vinywaji vya KVant Gin
vikitolewa bure mlangoni, Pia tutatoa Red roses na Rollypop kwa akinadada 100 wa kwanza watakauingia
Resort na viile vile zawadi kibao kushindaniwa siku hiyo” alisema
Wito kwa wakazi wa Jiji la Mwanza na
wageni wapenzi wa burudani wafike kujionea burudani mpya ya kiwango ambayo kwa
mara ya kwanza itaanza kutolewa kwenye madhari ya fukwe kwa mitindo tofauti kwa
kusherehekea na kufanya utalii kwa kingilio cha shilingi elfu kumi tu mlangoni
huku ulinzi wa wateja na mali zao ukiimarishwa kwa asilimia 100.
No comments:
Post a Comment