Tuesday, February 4, 2014

WATUMISHI WA MAHAKAMA MKOANI DODOMA WAMETAKIWA KUTENDA HAKI ILI KUTIMIZA MAJUKUMU YAO KWA JAMII.






Hayo yamesemwa na  Jaji mfawidhi Mkoani Dodoma  Crecencia  Makuru wakati akitoa ufafanuzi katika maadhimisho ya siku ya sheria nchini  yaliyo fanyika katika viwanja vya mahakama kuu mkoani Dodoma.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Jaji   Makuru amesema maudhui ya sheria ya mwaka huu ni utendaji haki kwa wakati .Sanjari na hayo  amesema kuna vitu vikuu vitatu vinavyo weza kusababisha mahakama kutoaminika ikiwemo ucheleweshwaji wa kesi.

Maadhimisho  hayo  ni ya kumi na nane tangu  kuanziswa kwa  maadhimisho hayo mwaka  1996.

No comments:

Post a Comment