Showing posts with label UCHUMI. Show all posts
Showing posts with label UCHUMI. Show all posts

Thursday, November 21, 2013

UWEPO WA WADHIBITI WENGI (REGULATOR​S) NI KIKWAZO KWA MAENDELEO YA SEKTA YA VIWANDA NCHINI - CTI

093
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Nchini (CTI) Bi Christine Kilindu (Mwisho Kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya viwanda nchini na mchango wa sekta hiyo katika kupambana na tatizo la ajira katika kilele cha Siku ya Viwanda Afrika, (Kati Kati) ni Kaimu Katibu Mkuu Odilo Otieno (Kushoto) Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) Emmanuel Kalenzi .
.Kesho ni kilele cha Siku ya Viwanda Afrika wananchi waombwa kujitokeza kwa wingi
.Tanzania yapiga hatua viwanda 700 vyaanzishwa ndani ya miaka mitano
.UNIDO yaifagilia serikali ya JK kwenye kuhamasisha uwekezaji kwenye sekta ya viwanda
.Ujasiriamali kufundishwa kuanzia mashuleni

Tuesday, October 16, 2012

MKUTANO WA KUHAMASISHA UTALII WAFUNGULIWA




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia alipofungua Mkutano wa kwanza wa  Kimataifa wa Kutangaza Utalii kwa Nchi za Bara la Afrika na Kuhamasisha Utalii Endelevu katika nchi hizo. 

Mkutano huo umefunguliwa leo Oktoba 15, 2012 katika Ukumbi wa AICC  leo Oktoba 15 Jijini Arusha na kuhudhuriwa na mawaziri 17 kutoka nchi mbalimbali za Afrika. Picha na OMR



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto) akipokea barua ya wazi kutoka kwa Katibu wa Mkuu wa Shirika la Utalii la Dunia, Taleb Rifai, iliyotolewa na Baraza la Waendesha Utalii Duniani (WTTC) mara baada ya kufungua Mkutano wa Kuhamasisha utalii barani Afrika leo, Oktoba 15, 2012, jijini Arusha. Katika Mkutano huo pia umehudhuriwa na Mawaziri 17 kutoka nchi mbalimbali za Afrika.Picha na OMR


                                        Makabidhiano yamekamilika