Daniel John Mapunda akiwa anasubiria kuingia studio.
Daniel akiwa na kazi zake.
Gerald Hando akiwa amesheheni bidhaa za kijana Danny. kwa mbaali Babra Hassa akiwa na shughuli zake.
Dk Isaac Maro, dk kijana aliye makini katika kazi zake.
Manager wa Choice FM na anchor wa Power Breakfast, akiwa amevurugwa, alinipotezea kumpiga picha akaniachia nywele tu!POLEEE
Baada ya kipindi mjadala wa pedi cure na manicure na kunyolewa dongo salon ulikua mzito kidogo, hapo ni Hando,Dk Isaac,Abel Onesmo wa pb on satoo na producer wa Power Breakfast Jimmy Francis wakimsikiza Dk akiwapa ukweli macho makavuuu!
Hando huyoooo na zawadi yake kutoka kwa kijana Danny amependezaje nalo! safi sana Danny, picha za kazi za Danny ziko hapo chini!
Kwa yeyote aendaye nje ya Tanzania, ingefaa abebe begi hili la rangi za nchi yetu! naona vazi la taifa limechelewa! Danny ameona fursa ameitumia je mwaonaje kama begi hili lita rasimishwa na kua sehemu ya nembo yetu kwa Taifa.?
Begi hilo hapo juu kwa nyuma linavyoonekana!
Made in Tanzania! kazi kwenu akina mama na akina dada
Kwa nyuma
Wow! niiiice, tafuteni sababu mnaovaa vitenge, ona linavyofanana, mechisheni
Kwa wenye Lap top begi hilo hapo
Muonekano tofauti
Thaminisha pande zooote
Begi lina mvuto vipi?
Mchanganyo wenye mvuto wa hatari! mi nimedata!
kazi ni kwako
Jamani jamani mi sina hali kwa kazi hii nzuri ya kijana Danny please! tumuunge mkono kwa kununua bidhaa zake na hata kumpa vitendea kazi!
DANIEL JOHN MAPUNDA, NI
MKAAZI WA KWA ALI MAUA HAPA DAR-ES-SALAA MWENYE UMRI WA MIAKA 22.
NI MJASIRIAMALI WA
KUTENGENEZA BIDHAA ZA HAND BAG,BEGI ZA KUSAFIRIA ZA SHULE ZA LAPTOP,NA ALIANZA MWAKA 2000, KAZI HIYO ALIJIFUNZA
KUTOKA KWA MJOMBA WAKE BWANA ALPHONCE.
MWAKA MMOJA BAADAE DANNY
ALISIMAMA KUTENGENEZA BIDHAA HIZO KUTOKANA NA KUKOSA NYENZO ZA KUENDELEZA KAZI
ZAKE.
BAADA YA KUISIKIA
KAMPEIGN YA MADE IN TANZANIA KUTOKA CLOUDS FM IKAMFANYA APATE TENA MORALI YA
KUANZA KAZI ZAKE KWA KUOMBA KUFANYIA KAZI ZAKE KWA RAFIKIYE AITWAYE KASSIM,
NAYE AKAMKUBALIA KUTUMIA OFISI ZAKE NA KILA KILICHOMO .
NA BAADA YA
KUZITENGENEZA BEGI ZAKE, MTAA MZIMA AISHIKO WAMEZIPOKEA VYEMA KWA KUZINUNUA.NA
KUMHAMASISHA ATAFUTE WAFADHILI WA KUMREJESHA SOKONI.
DANNY- O655 81 47 47
No comments:
Post a Comment