Mzee huyu anajaribu kupambana na mafuriko kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha huko SUDAN NA SUDAN KUSINI
Haijafahamika mara moja mama huyu maji haya alokua akiyachota ni kwa matumizi? Au ni katika harakati za kuyapunguza, huku mtoto wake akiwa amejishika tama.
Njia za kawaida hazipitiki,ukipata fursa kama hii ya kutembea msingini basi unatembea.
Kila mahali ni heka heka kukabiliana na maji yaliyosimamisha shughuli za raia wa Sudan Kusini.
Nyumba hii sijui ni full suti udongo? Au paa limeezuliwa? Lakini pi imezongwa kila upande! Majaaliwa ya wakaazi wake ni mashakani.
Kiila mmoja ni msarakambo
Nyumba yako mwenyewe unaikimbia! Maji ni nom asana! Yana power ya ajabu mnoo! Mzee haamini macho yake kwa akiona nacho!
Mchanga huu unachotwa na kwenda wekwa mahali kutengeneza tuta ambalo litafanya kingo kuzuia maji eneo linguine na kulikausha maisha yaendelee! poleni.
Miundo mbinu haifikiki na hivyo inabidi kilichoko karibu yako kiwe nyenzo muhimu.
Vivuko navyo vimesongwa kiasi cha kutishia usalama.
Kila mahali ni maji! Eneo pekee kavu ni barabarani!
No comments:
Post a Comment