Tuesday, August 6, 2013

WAFUASI WA RAIS MUGABE WASHEREHEKEA USHINDI





Wafuasi wa Rais Robert Gabriel Mugabe wa Zimbabwe, wamefanya sherehe kubwa kufuatia rais huyo kushinda katika uchaguzi wa rais uliofanyika mwishoni mwa mwezi uliopita nchini humo.
Wafuasi wa rais huyo, walifurika mabarabarani kwa wingi hapo jana wakisherehekea ushindi wa rais huyo. 

Kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi huo, Rais
Mugabe alishinda kwa kupata asilimia 61 ya kura zilizopigwa huku mpinzani wake mkuu Morgan Tsvangirai akipata asilimia 34 ya kura hizo.

Pamoja na chama cha MDC kinachoongozwa na Tsvangirai kupinga matokeo hayo, lakini Umoja wa Afrika AU umetoa taarifa yake kuhusiana na uchaguzi huo huku ukiisifu Zimbabwe kwa kuendesha uchaguzi huru na wa amani na kupinga tuhuma za kufanyika udanganyifu zilizotolewa na mgombea mkuu huyo wa upinzani nchini humo.

Mkuu wa timu ya waangalizi wa Umoja wa Afrika AU Olusegun Obasannjo alisema kuwa uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Zimbabwe siku ya Jumatano iliyopita ulikuwa huru na wa haki.

No comments:

Post a Comment