Marekani
imetangaza kuwa balozi zake katika nchi na sehemu 19 zilizoko Mashariki ya Kati
na Afrika zitaendelea kufungwa, ikiwa ni hatua ya kukabiliana na tishio la
shambulizi la kigaidi dhidi ya nchi hiyo.
Msemaji
wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Jen Pseki amesema kuwa, hatua hiyo ni
tahadhari dhidi ya shambulizi la kigaidi na pia unatokana na sikukuu ya Eid
el-Fitr. Amesema hatua hiyo haina lengo la kuongeza vitisho, bali ni tahadhari
na pia kuchukua hatua sahihi kulinda wafanyakazi wa balozi hizo.
Amesema
taarifa zinasema kuwa, kundi la Al Qaida naa makundi yenye uhusiano na kundi
hilo yanapanga kufanya mashambulizi ya kigaidi ambayo yanaweza kufanywa muda
wowote kuanzia sasa hadi mwisho wa mwezi huu.
aya bwana lakini hawa jamaa Al Qaida ni hatari kweli so mimi nawaunga mkono Marekani kwa hatua wanaopanga kuchukua ili kujihadhari zaid kwani siku hizi mambo mapya yamevamia Diplomasia na watu hawajui maswala ya kinga za kibalozi kwani mara nyingi tumesikia kuwa mabalozi mbalimbali wameuliwa bila kuangalia privilege na immunity zake. mfano juzi kati tu kule Libya tuliona balozi wa Marekani alivyouliwa.
ReplyDelete