Wednesday, August 21, 2013

MWANARIADHA OSCAR PISTORIUS APANDISHWA TENA KIZIMBANI , ASHTAKIWA KWA MAUAJI


Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amefikishwa mahakamani leo katika Mji wa Pretoria,Afrika Kusini na ameshtakiwa kwa kosa la kumuua mpenzi wake.
Mwendesha mashtaka wa Mahakama hiyo amemsomea makosa ya kumuua,Reeva Steenkamp kwa kumpiga risasi mpenzi wake usiku wa manane akiwa amejifungia katika choo nyumbani kwake.

  Dada yake Oscar aitwaye Aimee akilia mahakamani hapo

Akijitetea mahakamani hapo Mwanariadha huyo alisema kuwa alidhania ni mtu mwingine aliyejaribu kuingia kwa nguvu nyumbani kwake na hakumuua mpenzi wake kwa kudhamiria,ambapo upande wa mashtaka umesema mwanariadha huyo alipanga kumuua mwanamitindo huyo.
Marafiki wa marehemu Reeva wakilia mahakamani hapo 

Mmoja wa majirani wa Pistorius na ambaye ni shahidi alikiri kusikia mayowe ya mwanamke kisha milio ya risasi. Hata hivyo shahidi mkuu anayefahamu kilichotokea wakati huo ni mmoja tu naye ni Oscar Pistorius,ambapo polisi walisema kuwa kumekuwa na ugomvi wa mara kadhaa kati ya mshtakiwa na marehemu mpenzi wake.

Enzi za mapenzi na uhai wa Reeva Steenkamp

Oscar Pistorius alizingirwa na umati mkubwa wa waandishi wa habari alipofika mahakamani mji wa Pretoria. Akiandamana na jamaa wake mwanariadha huyo alifanya maombi maalum. Punde baada ya kusomewa makosa ya kumuua Mwanamitindo Reeva Steenkamp, Oscar alionekana kupatwa na huzuni kubwa.

Kesi hiyo sasa imehamishiwa mahakama kuu na itasikizwa mapema mwakani,na imehairishwa hadi mwezi Machi mwakani.
Pistorius anasifika kama mwanaridha wa kwanza mlemavu kushiriki michezo ya Olimpiki, habari za mauaji ya mpenzi wake Pistorius ziliwashangaza wengi Afrika Kusini kwani anasifika kama mwanaridha anayeiletea nchi hiyo sifa.

No comments:

Post a Comment