Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa
nchini (UNIC) Stella Vuzo akielezea jukumu lao kubwa wao kama UNIC ni
kuelimisha jamii ambapo kwa kufanya hivyo wamehamasika kuanzisha vilabu vya
kujisomea kwa shule za msingi vitakavyowajengea watoto msingi mzuri wa kupenda
kujisomea ili kufahamu mambo mengi zaidi yanayoendelea duniani katika nyanja ya
Sayansi, Teknolojia na habari.
Msaidizi wa Maktaba ya UNIC Harriet Macha ( wa tatu
kushoto) na Mkurugenzi wa Taasisi ya Soma Book Café , mshiriki katika
kuhamasisha uanzishwaji wa Klabu za Kujisomea mashuleni Mama Demere Kitunga (
wa nne kushoto) wakikabidhi vitabu vya kujisomea kwa walimu na baadhi ya
wanafunzi wa shule ya msingi Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) kwa
kushirkiana na Soma Book Café walihamasisha kuanzishwa kwa Klabu za Kujisomea
katika shule tatu za msingi ambazo ni Hananasif, Kumbukumbu na Oysterbay ili
kujenga tabia ya kujisomea kwa watoto tangu utotoni. Klabu ya Kujisomea ya
Shule ya Msingi Oysterbay imezinduliwa rasmi jana tarehe 31 Julai 2013 kwa
kukabidhiwa mashelfu na vitabu vilivyotolewa na Kituo cha Habari cha Umoja wa
Mataifa (UNIC), Soma Book Café pamoja na Book Aid International kupitia Maktaba
Kuu ya Taifa.
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa
nchini (UNIC) Stella Vuzo akishiriki zoezi hilo la kukabidhi vitabu kwa baadhi
ya wanafunzi wa shule ya Msingi Oysterbay wakihamasisha wanafunzi kujenga tabia
ya kujisomea tangu wakiwa wadogo.
Afisa Habari wa UNIC Usia Nkhoma Ledama naye alishiriki
zoezi hilo.
Mwalimu Salome Makanza (kushoto) akitoa shukrani kwa
kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) kwa msaada huo ambapo waliahidi
kuleta mabadiliko ya maendeleo kwa wanafunzi wao kujijengea tabia ya kujisomea
na hata kuongeza ufaulu kwa matokeo ya darasa la saba shuleni hapo. Katikati ni
Msaidizi wa Maktaba ya UNIC Harriet Macha na kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya
Soma Book Café , mshiriki katika kuhamasisha uanzishwaji wa Klabu za Kujisomea
mashuleni Mama Demere Kitunga.
Msaidizi wa Maktaba ya UNIC Harriet Macha akitoa ushauri
wa namna ya upangaji vitabu kwa Msimamizi wa Maktaba ya shule hiyo Mwl.
Veronica Kassidy.
Unic team wakijikumbushia baadhi ya vitabu walivyowahi
kuvisoma walipokuwa shule za msingi.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Oysterbay
wakichagulia vitabu vya kujisomea katika maktaba ya shule yao.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Soma Book Café , mshiriki katika
kuhamasisha uanzishwaji wa Klabu za Kujisomea mashuleni Mama Demere Kitunga na
Afisa Habari wa UNIC Stella Vuzo wakiteta jambo na baadhi ya wanafunzi wa shule
mara baada ya kumaliza zoezi la kukabidhi vitabu wanafunzi hao.
No comments:
Post a Comment