Monday, August 5, 2013

MKUU WA MKOA WA SINGIDA MHE. DR. PARSEKO V. KONE NA MKUU WA WILAYA YA BAHI MHE. BETTY MKWASA WATEMBELEA MABANDA YA WIZARA YA UCHUKUZI NA TAASISI ZAKE KATIKA MAONESHO YA NANENANE YANAYOFANYIKA KITAIFA DODOMA LEO MCHANA.

Mkuu wa Mkoa wa Singida akiweka sahihi kwenye kitabu cha wageni katika banda la Wizara ya Uchukuzi, wakati alipotembelea mabanda ya Wizara hiyo na Taasisi zake ,maonesho ya kitaifa ya kilimo yanayofanyika kitaifa mkoani Dodoma. Kauli Mbiu ya Mwaka huu ni "Zalisha mazao ya kilimo na Mifugo kwa kulenga mahitaji ya Soko'.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Parseko V. Kone (mwenye suti nyeusi) akisisitiza jambo kwa Afisa Mwandamizi wa Masoko wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Bi. Lydia Mallya (kulia), wakati alipotembelea banda la Mamlaka hiyo katika maonesho ya kilimo katika viwanja vya Nzuguni, Dodoma hana.
 
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Parseko V. Kone akisikiliza maelezo ya namna Chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT) kinavyotoa kozi zake kutoka kwa Afisa Udahili na Mitihani kutoka Chuo hicho, Bw. Benjamin Myaya(kulia), wakati alipotembelea banda la Chuo hicho katika maonesho ya Kilimo ya Nanenane yanayofanyika kitaifa Mkoani Dodoma katika viwanja vya Nzuguni.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Parseko V. Kone, akimsikiliza Kaimu Meneja wa Mipango, Usanifu na Tathmini kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA). Bw. Mbila Mdemu(aliyeshika fimbo), wakati mkuu wa mkoa huyo alipotembelea banda la Mamlaka hiyo lililopo katika maonesho ya Kilimo ya nanenane yanayofanyika kitaifa mkoani Dodoma. Kulia kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Betty Mkwasa.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Parseko V. Kone, akimskiliza Afisa Huduma za Abiria wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), Bw. Peter Ngwale(wa pili kulia) wakati alipotembelea banda la Mamlaka hiyo, katika maonesho ya Kilimo nanenane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nzuguni,Dodoma.

No comments:

Post a Comment