Tuesday, August 6, 2013

CHANGAMOTO YA UNYONYESHAJI TANZANIA




                                                                   Mama akinyonyesha mwanawe



Wakati wiki ya kimataifa ya unyonyeshaji ikiendelea, nchini Tanzania mkakati wa elimu kwa uma unakabiliwa na changamoto ya mawasiliano katika kuwafikia walengwa wakuu, ambao ni wanawake wanaonyonyesha.

Katika mahojiano maalum na idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa, naibu waziri wa wizara ya afya wa  Dk Seif Rashid amesema wizara ina mkakati wa kuongeza nguvu katika kutoa elimu ya afya kwa uma na kuongeza kuwa wengi wanaitikia wito wa kunyonyesha watoto kwa kuzingatia kanuni za afya.

No comments:

Post a Comment