Thursday, August 15, 2013

WAZIRI MWAKYEMBE AKABIDHI RASMI ITHIBATI YA MAFUNZO YA MIZIGO HATARISHI KWA NIT



Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe(aliyevaa tai nyekundu), akimsikiliza Mkuu wa Chuo Cha Taifa cha Usafirishani (NIT),Mhandisi Dk. Zacharia Mganilwa(kulia)  kabla Waziri huyo hajakabidhi Ithibati ya Kuendeshea mafunzo ya wahudumiaji wa Mizigo hatarishi katika viwanja vya NIT. Kushoto  kwa Waziri wa Uchukuzi ni Mwenyektii wa Baraza la Uongozi wa chuo cha NIT, Ms. Priscilla J. Chilipweli.


 Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, akitoa hotuba yake kwa wahitimu na wageni waalikwa, hawapo pichani wakati wa sherehe ya kukabidhi Ithibati  ya Kuendeshea mafunzo ya wahudumiaji wa Mizigo hatarishi katika viwanja vya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) .
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, akikabidhi Ithibati  ya Kuendeshea mafunzo ya wahudumiaji wa Mizigo hatarishi kwa Mhadhiri wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT), Bw. Juma Fimbo leo asubuhi wakati wa sherehe maalum za kukabidhi ithibati hiyo ziliyofanyika katika viwanja vya chuo hicho. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Chuo hicho Mhandisi Dkt. Zacharia Mganilwa(wa kwanza kushoto) na Mkuu Mwenyektii wa Baraza la Uongozi wa chuo cha NIT, Ms. Priscilla J. Chilipweli( wa pili kushoto).
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, akikabidhi Ithibati  ya Kuendeshea mafunzo ya wahudumiaji wa Mizigo hatarishi kwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa chuo cha NIT, Ms. Priscilla J. Chilipweli huku akishuhudiwa na Mkuu wa Chuo hicho Mhandisi Dkt. Zacharia Mganilwa(wa kwanza kushoto
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe (wa tatu kutoka kulia waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji(NIT), Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa chuo cha NIT Ms. Priscilla J. Chilipweli(kulia kwa Waziri Mwakyembe),  Mkuu wa Chuo hicho Mhandisi Dkt. Zacharia Mganilwa (kushoto kwa Waziri Mwakyembe) na wahitimu wa kozi ya kuhudumia mizigo hatarishi Bi.  Dorah John (wa kwanza kulia waliosimama) na Zuhura Adam (wa kwanza kushoto waliosimama) wakati wa sherehe za kukabidhi rasmi Ithibati  ya Kuendeshea mafunzo ya wahudumiaji wa Mizigo hatarishi pamoja na kutunuku vyeti kwa wahitimu wa kozi hiyo. Wa kwanza kulia waliokaa ni Mkurugenzi wa Huduma za Uchukuzi Wizara ya Uchukuzi, bw. Peter Lupatu.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-UCHUKUZI)
 

No comments:

Post a Comment