Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Assah Mwambene leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara hiyo amekanusha taarifa zilizoandikwa kwenye mitandao kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete ni shemeji wa aliyekuwa Rais wa Rwanda, marehemu Juvenal Habyarimana.
“Taarifa hizi siyo za kweli na nafikiri taarifa zimeandaliwa kwa ajili ya kumpaka matope Mheshimiwa Rais. Kama kuna taarifa zozote basi tunaweza kutoa ufafanuzi lakini taarifa hizo siyo za kweli na bahati mbaya zimeendelea kujirudia na zinatoka kwenye mitandao mingi hasa kutoka Rwanda,” amesema Mwambene na kufafanua kuwa lengo la mitandao ya kijamii ni kuhabarisha na kuelimisha umma wala siyo kupotosha jamii kwa kuandika habari zisizo na ukweli wowote.
Ili kukabiliana na taarifa potofu, Mwambene amesema, “...katika mabadiliko ambayo yanapendekezwa katika Serikali ya ku-deal na tatizo hili, tunakuja na pendekezo la kisheria ambalo litakalohakikisha kwamba tunamtamuba kila mtumiaji wa mitandao hii kwa mfano blog. Nafikiri mmeanza kuona kuna training sasa zinafaanyika kuhakikisha kwa mfano --- wote wenye blogu unakuta wengi siyo waandishi wa habari, hajasomea uandishi wa habari lakini blogu yake inafanya kazi kama gazeti --- tulichokifanya sasa na nafikiri tutaendelea mpaka uje utaratibu wa kisheria, tunamtambua kila mtumiaji wa iwe ni blog, iwe ni Twitter, iwe ni internet cafe...” alisema Mwambene.
No comments:
Post a Comment