Friday, August 23, 2013

LA LIGA IS BORING



kwa kumbukumbu ya haraka ligi kuu ya hispania imekuwa na mabingwa watatu pekee katika kipindi cha miaka kumi iliyopita ambao ni real madrid , fc barcelona na valencia .
valencia walitwaa ubingwa huu mara mbili wakiwa chini ya kocha rafael benitez lakini kinyume na hapo real madrid na barcelona ndio wamekuwa wakigawana mataji ya la liga baina yao .
msimu mpya wa ligi hii ulianza kwa matokeo ambayo hayakuwashangaza wengi, barcelona waliwafunga levante bao saba bila na mshangao pekee uliokuwepo ni kwa jinsi ambavyo real madrid wakiwa na kikosi kilichosheheni nyota walivyohangaikia ushindi wa mabao mawili kwa moja mbele ya real betis .
ushindi wa barca ulisababisha kocha wa atletico madrid kutoa kauli kuwa ligi ya hispania inaboa na sababu ya kauli hii ilikuwa jinsi ambavyo timu mbili za barcelona na real madrid zinavyotawala ligi hii pasipo kuwa na fursa halisi ya ushindi kwa timu nyingine kumi na nane .
sera ya michezo nchini hispania ina chembe chembe fulani za uonevu kwa vilabu vidogo, sera hii ambayo ilianza mwanzoni mwa miaka ya tisini ilitoa fursa kwa klabu za real madrid na barcelona pamoja na osasuna na athletic bilbao kuendeshwa kama klabu za wananchi au wanachama na hivyo kuondolewa mzigo wa kodi huku klabu nyingine zikilazimishwa kuendeshwa kama kampuni zenye kujiendesha kwa misingi ya faida na hasara .
hii imemaanisha kuwa uendeshwaji wa vilabu umekuwa mgumu sana kwa timu nyingine tofauti na barcelona na madrid ambazo kwa upande mwingine pia zinapata gawio kubwa la mkataba wa haki za matangazo ya televisheni .
msimu uliopita wakati rayo vallecano walipokutana na real madrid viongozi wa rayo waliwaonya wachezaji wao kuwa endapo wangebadilishana na jezi na wachezaji wa wapinzani wao siku hiyo wangekatwa mishahara yao midogo kufidia jezi hizo kwa kuwa klabu ina ukata mkubwa ,

 kabla ya hapo mgomo wa wachezaji wa klabu kadhaa nchini hispania ulitishia primera liga kusimama na dai kubwa la wachezaji lilikuwa mishahara ya zaidi ya miezi mitatu .
ukiangalia katika kipindi cha misimu miwili mpaka mitatu kumekuwa na mfuatano wa matukio ya wachezaji nyota wa timu ndogo za hispania kuikimbia ligi ya nchi hiyo .
juan mata , santi cazorla , nacho monreal ,            david de gea , david silva , jesus navas , alvaro negredo , roberto soldado na javi martinez  ni baadhi tu ya majina yanayotengeneza orodha ndefu ya wachezaji walioihama ligi ya hispania katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita na kukimbilia kwenye ligi nyingine .
ukijaribu kufananisha na ligi kama ya england utagundua kuwa wigo wa ushindani ni mkubwa zaidi na ushindani huu unazidi kuongezeka ukizingatia kuwa baadhi ya timu ambazo hutazamwa kama timu ndogo zimefanya usajili mkubwa ambao kwa mahesabu ya haraka utaleta changamoto ya ushindani .
nchini hispania imezoeleka kuwa wachezaji bora wote hucheza mojawapo kati ya timu hizi mbili za barcelona na real madrid mbaya zaidi kwa soka la nchi hii ni kwamba mazoea haya yamejenga mazoea mapya ya wachezaji wa timu nyingine kuhamia timu ambazo zitawapa nafasi ya kuwa washindi kwenye nchi nyingine kwa kuwa wachezaji wote nyota hawawezi kulundikana jijini madrid na huko catalunya ,
na hii ndio sababu ya kocha wa atletico madrid diego simeone kusema kuwa la liga is boring .

No comments:

Post a Comment