Tuesday, August 27, 2013

SEMINA YA FURSA KWA VIJANA YAFANYIKA LEO MKOANI SINGIDA

Mwakilishi wa Shiriki la NSSF kutoka Makao Makuu jijini Dar,Bwa.Salim Khalfan akielezea fursa mbalimbali zinazopatikana kwa mtu yeyote anayejiunga na shirika la NSSF,alifafanua hayo leo kwenye ukumbi wa Luluma,nje kidogo ya mji wa Singida,Salim alibanisha kuwa mtu yeyote atakayejiunga na shirika hilo atanufaika na mambo mengi,ikiwemo suala la matibabu,mikopo na mengineyo lukuki yanayopatikana ndani ya shirika hilo.Semina hiyo ambayo inafanyika ikiwa ni mkoa wa tatu huu,ikianzia Kigoma,Tabora na sasa Singida,iliandaliwa na Clouds Media Group na kufadhiriwa na shirika la NSSF,Zantel,MaxMalipo,Lake Oil.
 Pichani juu ni sehemu washiriki wa semina ya Fursa kwa vijana,wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikizungumzwa kwenye semina hiyo,ambayo imeonekana kuwavutia vilivyo kwa sehemu ya wakazi wa mji wa Singida waliojitokeza kushiriki. 
   Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba,akizungumza mbele ya washiriki wa Semina ya Fursa ndani ya ukumbi  wa  Luluma,nje kidogo ya mji wa Singida, kuhusiana na fursa mbalimbali wanazozipata vijana na kuhakikisha wanazitumia ipasavyo,aliongeza kuwa vijana wengi wamekuwa ni watu wa kulalamika lalamika tu na kukata tamaa mapema,aidha Ruge amewataka vijana kuwa na muamko wa kufanya kazi na kujituma kwa bidii pale fursa yoyote inapotokea.
 Mmoja wa Watangazaji mahiri wa Clouds FM,Millard Ayo akizungumza mbele ya vijana wenzake ,nama alivyobahatika kuzitumia fursa mbalimbali alizokuwa akizipata kwa ufasaha na kwa umakini mkubwa mpaka hapo alipo,anabainisha kuwa kilichompelekea hapo alipo mpaka sasa ni namna alivyojijenga kwa nidhamu,kujituma na bidii kubwa ya kazi kila alipokuwa akiipata fursa,aidha amewataka vijana wenzake kuacha tabia ya kukata tamaa mapema na kutokuwa wavivu wa kufanya kazi,kwani kwa kufanya hivyo maendeleo hayatapatikana kirahisi.
PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

No comments:

Post a Comment