Ni miaka nane sasa imepita tangu le
proffeseur arsene wenger alipokiongoza kikosi cha washika bunduki wa the
emirates arsenal the gunners kutwaa ubingwa wa aina yoyote ile .
ni miaka nane ambayo mashabiki wa
arsenal wamevumilia mengi , miaka nane ambayo timu kama man united , chelsea ,
manchester city , liverpool , swansea na hata wigan zimetwaa walau kombe moja
huku arsenal wakibakia wakiwa wa mafanikio.
mapema wakati dirisha la usajili
lilipofunguliwa arsenal ilihusishwa na usajili wawachezaji nyota kadhaa
wakiwemo stevan jovetic , marouane fellaini , wayne rooney , gonzalo higuain na
hivi karibuni luis suarez .
Gonzalo higuain alikaribia kabisa
kujiunga na arsenal baada ya kufikia makubaliano binafsi kimsingi kabla napoli
hajawafika na kuharibu mpango wote na kuwaacha the gunners wakishikwa na butwaa
.
Hivi karibuni tetesi zimehamia kwa
mshambuliaji wa kimataifa wa uruguay luis suarez ambaye arsenal wamepeleka ofa
mbili za kumsajili ya kwanza ikiwa paundi milioni 35 ya pili ikiwa ya paundi milioni 41 zote mbili
zikikataliwa na liverpool ambao wiki hii wamesema kuwa timu itakayomtaka suarez
ilipe paundi milioni 55 .
Siku chache zilizopita arsenal pia
walikuwa wakifuatilia suala la wayne rooney kwa ukaribu na mzee wenger kwa
kauli yake alisema kuwa kwa arsenal ina uwezo wa kumsajili mchezaji huyo na
hata kuondokana na urasimu wa sera za klabu za mishahara ya daraja la kati na
kumlipa rooney mshahara ambao utavunja rekodi ya klabu hiyo.
Kwa mujibu wa makadirio ya jarida la
forbes linalofanya utafiti wa masuala ya kifedha kwa makampuni na
wafanyabiashara mbalimbali duniani arsenal ni klabu ya nne kwa utajiri barani
ulaya nyuma ya real madrid , manchester
united na fc barcelona .
kama fedha iko kwanini arsenal
ishindwe kutwaa mataji ? hilo ni swali gumu , ukiangalia aina ya wachezaji
ambao arsenal imehusishwa na kuwasajili unapata maswali mengi kuliko majibu .
jovetic , suarez , rooney na higuain
wote ni washambuliaji , tofauti pekee ilikuwa kwa fellaini ambaye ni kiungo
mwenye nguvu .
Msimamo wa ligi kwa msimu uliopita
ambapo arsenal ilishika nafasi ya nne unaonyesha kuwa kufunga mabao halikuwa
tatizo la msingi lililoitatiza arsenal , lukas podolski , olivier giroud na
theo walcott na hata viungo kina santi cazorla na mikael arteta wameonyesha
uwezo mkubwa wa kufunga mabao na timu ilikuwa na wastani wa kufunga angalau
mabao mawili kila mechi , tatizo la arsenal haliko kwenye safu ya ushambuliaji
bali safu ya ulinzi , kwa maoni ya wachambuzi wengi arsenal inahitaji beki
shupavu kama ashley williams golikipa mwenye uwezo wa kutegemewa na timu kama
asmir begovic au julio caesar na kiungo mwenye mbavu nene ambaye atasaidia
Kukatisha mashambulizi ya timu pinzani na kuanzisha pasi fupi kwa kina cazorla
na jack wilshere wakafanye mambo yao kwenye kumi na nane ya mpinzani .
msimu wa kabla ya msimu uliopita
arsenal ilikuwa na mchezaji ambaye alishika nafasi ya kwanza kwenye chati ya
ufungaji kwenye epl , robin van persie , mabao yake yake 30 ambayo alifunga
kwenye timu iliyomaliza nafasi ya nne yanaonyesha picha halisi ya
kinachozungumzwa hapa ,
Ukweli wa mambo ni kwamba arsenal
imepoteza utamaduni wa ushindi uliokuwepo enzi za kina tony adams na martin
keown , klabu hii inahitaji wachezaji wenye njaa na hamu ya mafanikio kiasi cha
kuwaongoza wenzao kufikia kutwaa taji walau moja , kiukweli miaka nane ni mingi
sana kwa klabu ya nne kwa utajiri ulaya na duniani kwa ujumla .
Mashabiki wa arsenal wanaweza kununa
na kukerwa kwa klabu hiyo kumkosa gonzalo higuain labda na luis suarez lakini
kwa watu wanaotazama mchezo kwa jicho la tatu arsenal wala haiwahitaji
wachezaji hawa kiufundi arsenal inahitaji viongozi , watu wenye njaa , watu
ambao hawatashangilia kushika nafasi ya nne bali watu watakapambana kufa na
kupona kuhakikisha heshima iliyozikwa na vifusi vya maghorofa yaliyojengwa
kwenye eneo lililowahi kuitwa uwanja wa highburu ihamie kwenye uwanja mpya wa
the emirates .
No comments:
Post a Comment