Monday, August 19, 2013
SOGA
Ligi kuu za soka barani ulaya zimeendelea kwa wiki yake ya pili tangu kuanza kwake wiki iliyopita huku baadhi kama vile ligi ya england zikifungua msimu wake wa mwaka 2013/2014 kwa mara yake ya kwanza wikiendi hii . Liverpool ndio waliocheza mechi ya kwanza kwenye epl msimu huu wakiwakaribisha stoke city kwenye uwanja wa anfield . Liverpool waliondoka na pointi zote tatu wakiwafunga stoke kwa bao moja bila . mfungaji wa bao hilo pekee alikuwa mshambuliaji wa kimataifa wa england daniel sturidge .Aston villa walikuwa wageni wa arsenal huko emirates . Mwanzo wa ligi haukuwa mwepesi kwa washika bunduki hao baada ya kujikuta wakifungwa kwa mabao matatu kwa moja . wafungaji wa aston villa walikuwa christian benteke akifunga mabao mawili na antonio luna huku olivier giroud akifunga bao pekee la arsenal ambao walimaliza mchezo wakiwa kumi uwanjani baada ya mlinzi laureant kiscileny kuonyeshwa kadi nyekundu. Huko carrow road norwich city na everton walishindwa kutambiana huku kila mmoja akiwa mbabe baada ya kugawana pointi katika sare ya mabao mawili kwa mawili . Steven whitaker na ricky van wolfwinkel walifunga kwa norwich na ross barkley pamoja na seamus coleman wakifunga mabao ya everton. vijana wa paolo di canio sunderland walianza ligi kwa kipigo cha bao moja bila toka kwa fulham . bao pekee la mchezo huo lilifungwa na payim kasammi.Southampton ambao walifunga safari hadi huko hawthorns kucheza na west bromwich albion walipata ushindi wa bao moja bila . Mkongwe ricky lambert alifunga bao pekee la mchezo huo .huko london boleyn ground west ham united wakiwa nyumbani waliwafunga vijana wapya cardiff city kwa mabao mawili bila .wafungaji kwenye mchezo huo walikuwa joe cole na kevin nolan. uwanja wa liberty huko wales ndio ulioshuhudia mchezo wa mwisho kwenye epl kwa siku ya jumamosi ambapo mabingwa watetezi wa ligi hiyo manchester united walikuwa mzigoni kucheza na mabingwa wa kombe la capital one swansea city . mabao ya robin van persie na danny welbeck kila mmoja akifunga mawili yalitosha kuwapa united ushindi wa mabao manne kwa moja . kijana toka ivory coasty wilfred bonny alifunga bao pekee la swansea. katika mechi za jumapili tottenham hotspurs walipata ushindi wa bao moja bila dhidi ya crystal palace mfungaji wa bao hilo pekee akiwa roberto soldado .Na chelsea ambao walikuwa wakimkaribisha jose mourinho kwa mara ya pili waliwafunga hull city kwa mabao mawili bila . wafungaji kwenye mchezo huo walikuwa oscar na frank lampard .kwenye ligi ya ujerumani mabingwa watetezi bayern munich waliwafunga frankfurt kwa bao moja bila . mfungaji wa bao hilo pekee alikuwa mshambuliaji mario mandzukic . nao borrusia dortmund waliwafunga vijana wapya wa braunschweig kwa mabao mawili kwa moja . wafungaji wa dortmund walikuwa jonas hoffman na marco reus huku kevin kratz akifunga bao pekee la braunschweig. nao borrusia monchegladbach waliwafunga hanover 96 kwa mabao matatu bila . wafungaji kwenye mchezo huo walikuwa filip daems , kevin krammer , na max kruse .nurenberg na hertha berlin walitoka sare ya mabao mawili kwa mawili . nurenberg walifunga kupitia kwa josip drimic na hiroshi tiyake huku hertha wakifunga kupitia kwa sami allagui na ronny.huko hispania mabingwa watetezi fc barcelona walianza kwa kishindo wakiwafunga levante mabao saba kwa sifuri . wafungaji kwenye mchezo huo walikuwa lionel messi akifunga mabao mawili , pedro rodriguez naye alifunga mawili , dani alves , alexis sanchez na xavi hernandez .nao real madrid walipata ushindi wa mabao mawili kwa moja mbele ya real betis . betis ndio walioanza kufunga kupitia kwa jorge molina kabla ya karim benzema na isco hawajaifungia madrid mabao yao kwenye mchezo huo .mchezo kati ya valencia na malaga uliisha kwa ushindi wa bao moja bila kwa valencia . mfungaji wa bao hilo pekee alikuwa ricardo costa.athletic bilbao waliwafunga valladolid kwa mabao mawili kwa moja wafungaji wakiwa markel suasaeta na iker munian kwa bilbao huku patrick ebert akifunga bao pekee kwa valladolid. Nchini ufaransa monaco waliwafunga montpellier kwa mabao manne kwa moja . wafungaji wa mabao hayo walikuwa radamel falcao na emanuel reveilere akifunga mabao matatu .paris st germain waliendelea na mwendo wao mbovu wa ligi baada ya kubanwa mbavu na ajacio kwa sare ya bao moja kwa moja . benoit pedretti ndio aliwafunga ajacio bao lao huku edinson cavanni akifunga bao la psg.nchini italia mabingwa juventus waliwafunga lazio kwenye italian super cup kwa mabao manne bila . wafungaji wa juventus kwenye mchezo huo walikuwa paul pogba , giorgio chielini , stephan liechtensteiner na carlos tevez ambaye alikuwa akivaa jezi ya mkongwe alesandro del piero kwa mara ya kwanza tangu mkongwe huyo alipoihama juventus .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment