Viwanja vya mnazi mmoja vilibadilika na kuleta muonekano tofauti.
Stage kabla haijakaliwa ilionekana hivi
Ashers wakiingia shughulini, walipendeza na kuichangamsha sherehe maana walikua wanacheza hao hatari.
Patron na matron, flower girl na ballboy walipendeza sana.
Godfrey Monyo na Gadiyosa Lamtei wote wa makampuni tanzu ya IPP wakiingia katika eneo la sherehe kwenye viwanja vya mnazi mmoja, ambapo karibu watu 1000 walihudhuria!
Mr anda Mrs Monyo
Baadae bwa harusi alibadili muonekano, na huu ndo muonekano wake mpya!
Patron ndo huyo Mr Eligius
Mrs Eligius, matron wa shughuli.
Pamoja wakiwakilisha familia mbili!
Monyo akideka kwa mkewe Gadiyosa!
Mr n' Mrs Monyo wazazi wa bwana harusi
Familia ya bi Gadiyosa Lamtey na mwenye tai ya mistari ndiye baba mzazi wa Gadiyosa mzee Lamtei.
Mratibu wa sherehe nzima alikua ni Joseph Ndamallya.
Godwin Gondwe , Alikua ni mshereheshaji mkuu.
Nami bwana Monyo chini ya maelekezo ya bwana hozee Ndamallya alinitaka kuongoza baadhi ya matukio na ikawa hivyo.
Sam Mahela wa Itv, naye alikua sehemu ya mac walioshika kipaza sauti kuongoza sherehe kubwa na nzuri iliyofana kwelikweli.
Ma-Mc's wakiachiana kijiti, Sam akimpa maelekezo Mc Sunday wa ITV.
Fatma Almas Nyangasa akiwa na mumewe Dk Nyangasa, Fatma nae alikua na sehemu ya kusherehesha. wamependezaje?! na hasa shemeji langu la ukweeh Doktaaaaah.
Ndamallya sijui alikua anashangaa ama kusema nini, hapa akiwa amekaa na bwana harusi mtarajiwa Ruben Mchome, Mchome naye alikua ni Mc siku hiyo, panapo majaaliwa Ruben atamuoa Naima Shariff binti wa balozi, usiulize mengi zaidi subra na kuwaombea waifikie siku yao kubwa maishani, ila vikao vimeanza, tumsapoti bwana Mchome mpare wa ukweli na bi Naima Shariff wifi langu la ukweeeh.
Somoe Ng'itu mamaa ya burudani alitokelezeaje? dada hapo pembeni sikumuuliza jina! ila alipendeza na kuchangamka mno!ni kutoka Guardian ltd.
waliwahi kufanya kazi pamoja, Somoe na Paul Malimbo ambaye sasa yupo MCT.
Jikeki la haja lilikuwepo bila kusahau ndafu haiko pichani.
Keki ikikatwa tayari kwa kulishana!
PICHA ZINGINE ZITAFUATA, NAONA MTANDAO UNAZINGUA!
ongereni sana
ReplyDelete