Monday, November 19, 2012

MAMLAKA YA ELIMU NCHINI -TEA YAFANYA HARAMBEE



Mgeni rasmi katika matembezi hayo ya hisani alikua ni waziri nchi ofisi ya waziri mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dr Mary Nagu akikata utepe, kuanzisha matembezi hayo ya hisani kuchangia ujenzi wa mabweni 30 katika wilaya mbalimbali hapa nchini ili kuwaepusha wasichana na mimba za mapema. msafara ulianzia Mlimani City hadi Viwanja vya Chuo kikuu cha Dar-Es-Salaam.
Kabla ya Matembezi, Mgeni rasmi alipiga Picha ya pamoja na Mkurugenzi mkuu wa TEA Rosemary Lulabuka, na kulia kwa Mama Nagu ni mwenyekiti wa bodi ya TEA Dk Naomi Katunzi, Rebbeca Gyumi na balozi Faraja Kota.
Sylvia kutoka TEA akitoa salaam kwa mgeni malyuum, Dr Mary Nagu
Matembezi yakaanza! mdogo mdogo hadi katika Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar-Es-Salaam.
Safari iliendelea
Hawa Wanajieleza Wanatoka wapi na walichangia kiasi cha tsh 820,100/- fedha taslim.
Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Baobab wakisubiri maelekezo.
 Baada tu ya maelekezo wakaanza kujiachia! walichangamka hatari wao walichangia kiasi cha Tshs 1,000,0000. NA Risala juu.
Brass Band ya Magereza iliongoza Matembezi hayo ya hisani.
Mgeni rasmi Dr Mary Nagu yuko fit! alifanikiwa kumaliza mwendo.
Kutoka Kushoto Barnabas Elias wa THT , Sylvia wa TEA na msaidizi wa Dr Mary Nagu.
Raha iliyoje Wana nguvu na Afya na furaha juu yake! wanakotokea soma bango.
Rosemary Lulabuka mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania akitoa salamu za ukaribisho.
Dr Mary Nagu waziri nchi ofisi ya waziri mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji akizungumza na wadau wa Elimu kuchangia.
Shemeji  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akiteta na Mkewe Faraja kota nini cha kuchangia, na alichangia (AHADI THS 12M) HONGERA SANA KWA MOYO WENU WA UTOAJI BWANA NA BIBI NYALANDU!
Burudani kutoka THT ilikuwepo na Balozi wa Kiswahili Barnabas Elias alikuwepo kuongoza kikosi cha burudani.
Baobab wao walicopy wimbo wa WE ARE THE WORLD Kwa ustadi mkubwa na tungo zao kadhaa waliimba!
Mwana Blogg ya 8020Fashions, Shamim Mwasha a.k.a ZEZE akikagua ubora wa picha! naye alikuwepo na ametupiamo mipicha tele.
Nami nilikuwepo! kwa heshima si nikavua kofia! du tunywele tumeparanganyikaje?! hahahha huu mdada wa kwanza blackbeauty hua ananichokoza sana! camera yake inaninyanyasa mno! natamani kujua blogg yake na jina limentoka kidogo! nadhani ni Mariam? maybe. NAOMBA KUWASILISHA KAMA UNAHITAJI KUINUA ELIMU NA MABWENI YAJENGWE CHANGIA ELIMU KWENDA 15564 AMA MPESA NI 404040 UTAKUA UMESAIDIA SANA, AMA KAMA UNA VIFAA VYA UJENZI PELEKA KATIKA OFISI ZA TEA MIKOCHENI JIJINI DAR-ES-SALAAM KARIBU NA ROSE GARDEN BAR

No comments:

Post a Comment