Shirika la reli nchini Kenya limezindua
treni mpya ambayo ina mwendo wa kasi ili kutoa huduma kwa wakaazi wa viungani
mwa mji wa Nairobi.Ni treni ya kwanza ya aina yake kuzinduliwa tangu Kenya
kujipatia uhuru mwaka 1963.
Treni hiyo itatoa usafiri kati ya
mji mkuu na mtaa wa Syokimau na viunga vyake, viungani mwa Nairobi ambako
serikali imejenga kituo cha treni ambacho ni cha kwanza kukamilishwa chini ya
mradi wa ukarabati wa mfumo wa reli ambao unafanyika kwa mara ya kwanza kwa
miaka 80.
Treni hiyo inanuiwa kupunguza
msongamano wa magari mjini Nairobi ambao ni mojawapo ya miji unaokuwa kwa kasi
barani Afrika ukiwa na watu zaidi ya milioni tatu.
Rais Kibaki aliyefungua rasmi kituo
hicho, alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuipanda treni hiyo.Kituo cha treni
cha Syokimau ni cha kwanza cha aina yake nchini Kenya, kikiwa na mashine za
elektroniki zinazokagua vyeti vya usafiri, pamoja na skirini kubwa ambazo
zinatangaza safari za treni.
Kila behewa lina uwezo wa kubeba
abiria sabini pamoja na miamoja na ishirini watakao simama.Huduma hiyo itakuwa
ya kasi na bora zaidi ikilinganishwa na treni za hapo nyuma na pia zitatumia
njia tofauti ya reli.
Safari ya kutoka mtaa wa Syokimau
inachukua dakika kumi na tano kwa treni hizo huku ikiwa mtu atakwenda kwa gari
itamchukua hata masaa mawili. Itamgharimu abiria shilingi miambili kwenda na
kutoka mjini.
No comments:
Post a Comment