The Diamonds hit maker’ Rihanna anaonekana ataandika vyema tarehe za mwaka huu kwenye diary yake kwa sababu kila kukicha anazidi kufanya makubwa katika career yake na anazidi kuweka historia kwa kufanya hit songs.
‘Diamonds’, wimbo wa kwanza kutoka kwenye album yake ‘Unapologetic’ inatarajia kupanda hadi nafasi ya kwanza kwenye Billboard Hot 100 ya wiki ijayo, hii itamfanya RiRi awe amefikisha idadi ya nyimbo 12 zilizoshika nafasi ya kwanza kwenye Billboard Hot 100, idadi inayomfanya alingane na mwanamuziki mkongwe Madonna katika historia ya miaka 54 ya chart hiyo.
Kwa mujibu wa Billboard, Rihanna sasa hivi amezidi kusogea juu kwenye idadi ya wanamuziki waliowahi kuweka nyimbo nyingi katika nafasi ya kwanza ya Billboard (most Hot 100 chart toppers of all time), ambapo anashikilia nafasi 20, Mariah Carey nafasi ya 18, na Michael Jackson nafasi ya 13 wakichukua nyimbo alizofanya M.J kama solo.
Kwa kulinganisha na umri wa the R&B Diva ikiwa ni miaka 24 na anatoa album mpya karibia kila mwaka, kama ataendelea na mwendo huu inawezekana akawafunika wote waliotajwa hapo juu, may be.
Kwa hiyo kama ni hivyo huenda Rihanna akamfikia Michael Jackson siku za usoni kwenye record ya Billboard top 100 kama akiendelea na mwendo huu hadi kuufikia umri aliofikia the King of Pop Michael Jackson.
Rihanna amekuwa the fastest female solo artist kujikusanyia nyimbo 12 zilizofika nafasi ya kwanza kwenye Billboard Chat 100 ndani ya miaka sita na miezi saba tu.
Baadhi ya ngoma za the R&B Diva RiRi zilizowahi kushika nafasi ya kwanza kwenye chat hiyo ni ile ya kwanza ‘SOS’mwaka 2006 ambayo ilidumu kwa muda mrefu, ‘Live Your Life’ iliyokaa wiki sita, ‘Umbrella’ wiki saba, ‘We found Love’....na Diamond ambayo imei-overtake “One More Night” ya Maroon 5's ubiquitous iliyokaa hapo kwa muda wa wiki tisa.
Well done Rihanna ila kumfikia Michael Jackson inahitaji uendelee kutoa hit baada ya hit design ya Diamonds hivi.
No comments:
Post a Comment