Wednesday, November 28, 2012
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA SHULE YA MSINGI YA KIROMO-MJINI BAGAMOYO
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simu za Mkononi, Sam Elangalloor, wakifunua kitambaa kwa pamoja kuashiria uzinduzi wa Shule ya Msingi Kiromo, iliyopo Wilaya ya Bagamoyo-Mkoa wa Pwani, iliyokarabatiwa na Kampuni ya Airtel Tanzania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simu za Mkononi, Sam Elangalloor, wakati akionyeshwa madawati yaliyotolewa na Kampuni hiyo kwa Shule ya Msingi Kiromo, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Shule hiyo baada ya kukamilika kwa ukarabati.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simu za Mkononi, Sam Elangalloor, kuhusu matumizi na makusudio ya mafunzo ya Kompyuta wakati alipotembelea katika chumba cha Kompyuta,
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simu za Mkononi, Sam Elangalloor, kukagua maeneo ya Shule ya Msingi Kiromo, wakati wa hafla ya uzinduzi wa shule hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Sam Elangalloor, wakati alipokuwa akitembelea katika Chumba cha Maktaba cha Shule ya Msingi Kiromo, baada ya uzinduzi rasmi wa shule hiyo, uliofanyika jana Nov 27, 2012.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment