M23 wakiondoka Goma
Kufuatia
juhudi za kimataifa na mataifa jirani, hatimaye waasi wa M23 katika Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo wamekubali kuondoka Goma na sasa wanakwenda kujikusanya
kwenye mji wa Sake, nje kidogo ya Goma.
Akizungumza
na DW, msemaji wa wapiganaji wa M23, Kanali Kazarama Vianeyi alisema tayari
wanaanza kuwaondoa wapiganaji wao katika wilaya ya Masisi, na kuwapeleka katika
mji wa Sake ulioko kilomita 27 kusini magharibi mwa mji wa Goma.
Akijibu
swali kuhusu ni lini wataanza kuwaondoa Goma wapiganaji wao, kanal Vianey
Kazarama alisema kujiondoa huko kutafanyika hatua kwa hatua.
Wakaazi wa
mji wa Goma wameeleza kuwa usiku wa kuamkia leo waliyaona magari ya
wapiganaji wa M23 pamoja na vifaa vya kivita bila yakujua wanaelekea wapi.
No comments:
Post a Comment