Nilishamomba msamaha siku nyingi kwamba niko kwenye mafunzo ya kupiga picha naomba tena mnisamehe! mwanga ulinisumbua lakini hapa Padre wa kwanza kushoto anatokea Jimbo katoliki Singida Padre Makalla alikuja parokiani kwetu kwa shughuli za kichungaji na kulia ndiye paroko wa parokia yangu ya Mt Peter Claver Padre Ivan.
Baadhi ya waumini wa Parokia ya Mt Peter Clavier waliokwenda kuwatembelea watoto hao.
Hii ni sehemu ya akina baba kwa uchache, mpiga picha bado kabisa, mvumilieni kwani hata mbuyu ulianza kama mchicha.
Sehemu ya mabinti wa betsaida , ambao wapata 95 wanaolelewa kituoni hapo.
sehemu ya zawadi kwa binti zetu wa BETSAIDA iliyoko Mbezi Louis nje kidogo ya mji, na utaratibu huu ni wa kawaida wa Parokia na jumuia zake Kuwatunza mabinti hawa baada ya Mwadhama Cardinal Polycalp Pengo kutupa bahati ya kuwahudumia, na hivyo kuuishi ukristo wetu kwa kuwajali wenye uhitaji,
Ikumbukwe kutoa ni moyo na si Utajiri, na maandiko yanasema Yatima na Wajane ni mboni ya jicho la Mungu unapowajali na kuwasaidia UTABARIKIWA, ukiwatupa na kuwanyanyasa UTALAANIWA.
Sehemu ya zawadi.
Hawa ndo mabinti tuliowaendea! wana ufahamu wa hali ya juu sana, Padre Muongoza Ibada aliwataka kwenda na sayanzi na Teknologia ambayo aliyaita mabadiliko ya kiulimwengu na malimwengu, akwasisitiza katika hilo kua na subra na kua na kiasi ili kuutetea usichana wao na kuwataka wasikubali kuishia kidato cha nne kwani siku hizi hakina dili bali wajibidiishe hadi ngazi ya chuo kikuu.
Mabinti hawa wanalelewa na masista wa mashirika mbalimbali ya kutoka ndani na nje ya nchi na hapa sister akipanga sehemu ya zawadi , ingawa jina sikulipata mara moja.
Sehemu ingine ya waumini.
Doreen Shio mwenyekiti wa WANAWAKE WAKATOLIKI Parokia ya Mt Peter ClAVIER
Erica WAWATA mwaminifu akiwa amempakata Gabriel a.k.a MPENZI huniita hivyo! Mwanangu wa mwisho.
Mrefu kuliko wote hapa anaitwa Engeneer Mabula yeye yuko kwenye kamati ya ujenzi ya Parokia, ametusaidia sana kwenye hilo, asante baba.
Zawadi zikibarikiwa kabla ya matumizi.lazima watoto wapate chakula chenye upako.
Viongozi wa Parokia akiwemo Makamu mwenyekiti wa Parokia mr Nchimbi aliye jirani na mti wakihakiki pesa zilizochangwa na manunuzi. vitu walivyopelekewa zawadi watoto viligharimu tshs 1.500.000/- na pesa taslimu walizokabidhiwa ni tshs 1,000,000/-.
Mwenye mic ni Mr Adam Kagoye mwenyekiti wa walei Parokia ya Mt Peter Clavier akielezea kidogo juu ya utamaduni wetu wa kujitolea.
Sister mkuu mlezi wa kituo akipokea mfuko wa zawadi kama ishara ya kupokea zawadi za waumini wa Parokia yangu.
Wanaume wakatoliki pia walitoa zawadi ya eneo la kusomea masomo iliyotengenezwa kwa mabo safi ya mninga, mwenye thirt ya njano ni mwenyekiti wa wanaume wakatoliki Mr Mruma.
Kwa upande wa dini katekista huyu hua anahakikisha mabinti zetu wanapata masomo husika na malezi ya kiimani.
Changamoto kubwa iliyoko kituoni hapo ni tatizo la maji baada ya pampu ya kisima hiki kuzama katika tope chini na ili kuweza kuinanua ama kupata kisima kingine basi zinahitajika kama kiasi cha milioni tano kurudisha huduma ya maji kituoni hapo ili kuimarisha mazingira, mbogamboga amabzo kwa kukosekana kwake watoto huishiwa damu na mazingira kunyauka, kwasasa jirani yao amabaye ni msamaria mwema huwaruhusu kuchukua maji kwake. TAFADHALI KAMA UNAWEZA KUSAIDIA KATIKA HILI TAFADHALI KARIBU NIKUFIKISHE KWENYE UONGOZI WA PAROKIA ILI KUWASAIDIA WATOTO HAWA NA MUNGU AKUBARIKI.
Mshkaji anaitwa Joshua yaani huyu ni Masanja ama joti hata nichokeje hua ananifurahisha mno!
Huyu ni KEONA binti yangu wote walikuwepo katika zoezi hilo la kuwatembelea mabinti zetu wa BETSAIDA ILIKUA NI JUMAMOSI ILIYOPITA.
No comments:
Post a Comment