Wednesday, November 28, 2012

KUMBE MSANII JOHN S. MAGANGA ALIFANYIWA UPASUAJI KIMAKOSA KABLA YA KIFO CHAKE


JOHN S. MAGANGA

 
                              Mwili wa John ukiwa umebebwa na wasanii wenzake.
                                            Wasanii wakimlilia John
Nape Nnauye katibu wa siasa na uenezi wa chama cha mapinduzi akizungumza msibani.
Nape akimpa pole baba mzazi wa John

 Msanii wa maigizo John Stephan amezikwa kwenye makaburi ya Kinondoni kufuatia kifo chake kilichotokea tarehe 24 Nov 2012 baada ya kuugua kwa muda mfupi. Akieleza mkasa mzima kupitia kipindi cha Take One Action cha Clouds TV, Baba mdogo wa marehemu ambaye pia ni msanii wa maigizo Deogratias Shija alisema marehemu alilazimika kufanyiwa upasuaji hospitali ya Mwananyamala baada ya kuonekana utumbo wake umetoboka.
Baada ya upasuaji kukamilika, daktari aliwaambia (Baba wa marehemu ) kuwa mashine za kumsaidia mgonjwa kupumua zina matatizo hivyo wamfanyie 'transfer' kwenda Muhimbili kwa matibabu zaidi.Walipofika Muhimbili John aliingizwa kwenye chumba maalumu kwa uchunguzi zaidi. Baada ya dk 10 daktari alitoka na kueleza kuwa tatizo alilokua nalo John siyo utumbo kutoboka kama madaktari wa Mwananyamala walivyodhani, bali kongosho lilishindwa fanya kazi vizuri hivyo likawa linavujisha maji kwenye tumbo ndiyo maana akawa anahisi maumivu makali na tumbo kujaa.

Hata hivyo mtaalam wa tatizo hilo la kongosho hakuwepo kwa wakati huo, hivyo John alitakiwa kulazwa hadi siku iliyo fuata ambapo mtaalam huyo angekuwepo. Siku hiyo Baba mdogo wa marehemu (Shija) alifika Muhimbili asubuhi ambapo aliambiwa asubiri kidogo kabla ya kujuzwa hali ya mgonjwa wake.
Baada ya dk chache daktari alitoka na kumueleza John amefariki.

1 comment:

  1. i cant believe it. jamani he was my hostel mate 2007 Near NBC Bnk.mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi

    ReplyDelete