Mshindi wa EBSS2012 Walter.
Shindano la kumsaka Epic Bongo Star limefikia tamati na Walter Chilambo ndiye mshindi na kunyijakulia kitita cha Tshs. Mil 50. Fainali ya shindano hilo lilikutanisha washiriki watano waliofikia hatua hiyo baada ya kuwabwaga wenzao lukuki toka mikoa mbalimbali ya Tanzania.
Washiriki walio fanikiwa kuingia hatua ya tano bora ni Nsami Nkwabi, Walter Chilambo,Salma Yussuf Abushir, Wababa Mtuka na NshomaNghangasamala. Baada ya hapo Nsami Nkwabi na NshomaNghangasamala walichujwa na kubaki Walter Chilambo,Salma Yussuf Abushir na Wababa Mtuka katika tatu bora.
Watatu hao walipanda jukwaani na kuimba wimbo mmoja kila mshiriki. Wababa na Walter waliendelea kukonga nyoyo za mashabiki, walishangiliwa sana na kutunzwa pia. Baada ya hapo mchujo ukapita tena. Safari hii Wababa Mtuka alitoka na kubaki washiriki wawili ambao ni Salma na Walter.
Wawili hao walipanda jukwaani na kuimba wimbo mmoja mmoja. Walter ndiye aliyepata shangwe kwa wingi sana toka kwa mashabiki. Mara hii Walter aliimba wimbo wa msanii Ben Paul ‘Nikikupata’ na kuutendea haki na kusababisha msanii huyo (Ben Paul) kumkubali Walter, hii ni kwa mujibu wa taarifa toka kwa washereheshaji (MCs) wa shughuli hiyo.
Kabla ya mshindi kutangazwa msanii wa bongo fleva Richie Mavoko alipanda jukwaani akifuatiwa na Ommy Dimpoz ambao walifanya show za nguvu.Baada ya hapo washiriki hao wawili waliitwa jukwaani na kitita cha Tsh. Mil 50 pia kililetwa jukwaani kikiwa ndani ya sanduku dogo jekundu na lilifunuliwa ili kuwathibitishia wananchi kuwa hela hizo zipo ndani ya sanduku hilo.
Ndipo Walter Chilambo alipotangazwa kua ndiye mshindi wa EBSS 2012.
No comments:
Post a Comment