Wednesday, November 21, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA MPANGO WA MIAKA MINNE WA ‘KUONA NI KUAMINI’ WA KUBORESHA AFYA YA MACHO KWA WATOTO KWA NCHI ZA KENYA, UGANDA NA TANZANIA.




 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa  Dkt. Paulina Mvella, wakati akimpima mtoto, Brayan Paul (7) mkazi wa Kigamboni, wakati Makamu alipokuwa akitembelea katika Mabanda kujionea shughuli za upimaji macho kwa watoto, wakati wa uzinduzi wa Mpango wa miaka mine wa ‘Kuona ni Kuamini’ .


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa  Daktari Bingwa wa (kulia) macho wa Watoto, kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, ‘Optometrist’, Judith Mwenda, wakati Makamu alipokuwa akitembelea katika Mabanda kujionea shughuli za upimaji macho kwa watoto, wakati wa uzinduzi wa Mpango wa miaka mine wa ‘Kuona ni Kuamini’ maalum kwa ajili ya kuboresha afya ya macho kwa watoto kwa Nchi za Kenya, Uganda na Tanzania, uliodhaminiwa na Benki ya Standard Chartered, uliofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, Nov 20, 2012.  Kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, Agrey Manry, (wa tatu kushoto) ni Mtoto Abubakar Siaba Kaim, mkazi wa Keko Mwanga, akipimwa macho. 



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa uzinduzi wa Mpango wa miaka mine wa ‘Kuona ni Kuamini’ maalum kwa ajili ya kuboresha afya ya macho kwa watoto kwa Nchi za Kenya, Uganda na Tanzania, uliodhaminiwa na Benki ya Standard Chartered, uliofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini maalum ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Mpango wa miaka minne wa ‘Kuona ni Kuamini’.

Shughuli ya upimaji wa macho kwa watoto, ikiendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, wakati wa uzinduzi wa mpango huo, .

No comments:

Post a Comment