Friday, November 9, 2012

KAMPENI YA UTOAJI HUDUMA KWA JAMII YAZINDULIWA


Chama cha madaktari wanawake Tanzania MEWATA jana kilizindua kampeni ya utoaji wa huduma mbalimbali za kiafya kwa jamii ikiwemo zoezi la uchunguzi wa saratani ya matiti,afya ya kinywa, saratani ya mlango wa uzazi,clinic kwa wanawake na watoto, upimaji wa macho  kwa wanawake katika mkoa wa Dar-Es-Salaam zoezi ambalo lilipata mwitikio mkuwa wa jamii kuchunguzwa afya zao.
Mgeni rasmi alikua mama Salma Kikwete First Lady, aliyewataka watanzania kuacha uvivu wa kucheck afya zao mara kwa mara.kushoto kwake ni Naibu Mwakilishi  wa mkuu wa mkoa  na kulia kwa mama ni Dr Sarafina Mkuwa mwenyekiti wa chama cha madaktari wanawake Tanzania a.k.a MEWATA.



Banda la Wide Spectrum wao walitoa msaada wa madawa kwa jamii, nao ni wasambazaji wakubwa wa madawa ndani na nje ya Dar.

Hawa ndugu ndo kutoka Wide Spectrum wakatikati ni Managing Director wa kampuni hiyo ya madawa ya binaadam Dr Hamza.
Mwenyekiti wa kwanza wa MEWATA na mwanzilishi  wa chama hiki mwaka 2005 kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani kampeni kubwa ilifanyika katika mkoa huu wa Dar-Es-Salaa,  kwa  sasa ni mkuu wa hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dr Marina Aloyce Njelekela, alikuwepo na hapa akifanyiwa mahojiano na Ufoo Saro wa ITV NA REDIO ONE.
Dr Sarafina Mkuwa ambaye ndiye mwenyekiti wa chama cha madaktari wanawake Tanzania akiongea na waandishi wa habari hawamo pichani.ila wanawakilishwa na vitendea kazi vyao.
kwa ufupi watu kadhaa walipata huduma kama ifuatavyo! Opthalmology -145
                                                                                               Dental              - 116
                                                                                               Cancer                  93
                                                                                         Breast cancer         - 175
                                                                                         Antenatal clinic          25
                                                                                                  Pediatrics         100
                                                                                                  Youth                   27
                                                                                                   bp                     221
na kufanya jumla ya wakaazi wa Dar-Es-Salaam wapatao 901 kupata huduma  za bure isipokua huduma za macho zilitolewa kwa gharama nafuu. HONGERA SANA MEWATA.



Mama huyu wa kimaasai alikuja akiwa tayari ana uchungu! alifanikiwa kumsalimia mama Kikwete pengine alitamani kumwambia hali yake, lakini mama hakujua, lakini alipata huduma stahiki kwa kuwahishwa hospitali, BIG UP MEWATA!


Huduma ya mama na mtoto ilipatikana katika viwanja vya mnazi mmoja, yaani ilikua hekaheka tangu saa nne asubuhi hadi saa kumi na moja jioni madaktari wa MEWATA hawakupata nafasi ya kupumzika.


                                            Huduma kwa wote zilitolewa.

Mabanda yalipangwa hivi na yote kidogo kidogo yakaja kufurika, hapa ilikua saa nne asubuhi.


Huwezi kufanya yote kwa wakati mmoja, kuongea wewe na picha upige wewe! aaagh wapi matokeo ndo haya! naomba radhi waungwana.
Tathmini ya shughuli ni muhimu kutoka wizara ya afya na mewata wakizungumza mawili matatu.


Mwenye miwani ni Dr Zaituni Jembe la MEWATA, kiukweli anachapa kazi na hana papara,msikivu na hujishusha ili kujifunza, asante Dr Zaituni.



Waandishi kazini, wakiwa wamemzunguuka mwenyekiti wa Mewata dk Sarafina Mkuwa, ili kupata story, na wametakiwa na mlezi wa MEWATA Mama Salma kikwete,  kuziweka hizo story Front Page na sio ndani.

                                                           Ulinzi ka kawa


Ukiwafikisha wakubwa wanakostahili lazima ushukuru! jamaa hapa ameinua kichwa naamini anamshukuru Mungu.
                                        Inawezekana hii tukutuku ndo kitendea kazi chake.

CHAMA CHA MADAKTARI WANAWAKE TANZANIA KINATARAJIA KUFANYA MKUTANO WAKE MKUU WA 13 WA NA  MWAKA NA  WA KISAYANSI KESHOTAREHE 10 NA 11 NOVEMBER JIJINI DAR-ES-SALAAM KAULI MBIU YAKE NI 'USHIRIKI WA WANAUME KATIKA KUBORESHA AFYA YA UZAZI NA MTOTO AFRIKA: TUKO WAPI?. NA UPIMAJI MWINGINE MKUBWA UTAFANYIKA MWEZI MARCH MWAKANI PANAPO MAJAALIWA, TAREHE NA MAHALI PA MKUTANO ENDELEA KUFUATILIA VYOMBO VYA HABARI,TV,REDIO,MAGAZETI NA BLOGS.

No comments:

Post a Comment