Wednesday, August 14, 2013

SOGA





soka ni mchezo wa vijana , wachezaji karibu wote unaowaona waking’aa hii leo mathalani lionel messi , cristiano ronaldo , robin van persie , edin hazard na wengine wengi ni zao la mipango ya muda mrefu ya kuzalisha na kuendeleza vipaji vya soka .
hakuna mahali ambako falsafa hii inaendelezwa kama nchini uholanzi ambako vijana wamekuwa wakiendelezwa na kujengwa kabla ya kuja kuliteka soka la dunia hii .
wakati ligi kuu za soka barani ulaya zinaanza mwishoni mwa wiki iliyopita macho ya wengi yalikuwa nchini ujerumani na ufaransa kuangalia kinachoendelea kati ya bayern munich , borusian dortmund , paris st german na monaco hakuna aliyetupia jicho kilichokuwa kinataka kuonekana kwenye soka la uholanzi .
zikiwa zimepita siku nne tangu ligi hizi zimeanza rasmi ulimwengu wa soka umetambulishwa kipaji kipya cha kijana mwenye umri wa miaka 17 huyu si mwingine bali ni kijana mbelgiji mwenye asili ya morocco.

bakali alifunga mabao matatu kati ya matano kwenye mchezo wa kwanza wa ligi kati ya timu yake ya psv eindhoven na nec na wiki iliyofuata amekuwa gumzo kwa wapenzi wa soka duniani kote .
alichokifanya bakalli sio kipya machoni kwa wanasoka wengi na ameingia kwenye ulimwengu wa soka kwa staili ambayo nyota wengi kabla yake waliwahi kuitumia kutambulisha vipaji vyao machoni kwa watu wakiwa na umri mdogo

alesandro del piero kabla ya kuwa gwiji wa juventus na timu ya taifa ya italia alifunga mabao matatu kwenye mchezo baina ya timu yake juventus na reginna , ukiwa mchezo wake wa kwanza akiwa kwenye kikosi cha kwanza na kilichofuata baada ya hapo ni lundo la medali za ligi ya serie a , uefa champions league pamoja na kombe la dunia akiwa na azzuri nazionale.
jina la pele ndio jina maarufu kuliko yote katika ulimwengu wa soka , mbrazil huyu alianzia kule kule alikoanzia bakali wiki iliyopita . pele alifunga mabao matatu kwenye mchezo wa nusu fainali ya kombe la dunia akiwa na umri wa miaka kumi na saba na mabao yake yalikuwa sehemu ya mabao matano yaliyoiua ufaransa kwenye kombe la dunia mwaka 1958 .
 baada ya hapo pele aliishia kuwa mchezaji bora kuliko wote waliowahi kutokea akiiongoza brazil kutwaa mataji mengine mawili ya dunia , na kuweka rekodi ya kufunga mabao zaidi ya elfu moja akiwa na klabu yake ya santos na timu ya taifa .
mshambuliaji jeremy menez naye anaingia kwenye orodha . mchezaji huyu ambaye ameng’aa akiwa na paris st germain na kwa  mara kadhaa akiwa na timu ya taifa ya ufaransa alianzia soka lake sochaux na ligi ya ufaransa ilipata picha halisi ya uwezo wake kwenye mchezo kati ya sochaux na bordeaux mwaka 2005 wakati akiwa na miaka 16. mabao haya matatu aliyafunga ndani ya dakika saba pekee.
mshambuliaji ambaye kwa sasa jina lake limetajwa sana kwenye tetesi za usajili wayne mark rooney hakupewa jina la the white pele bure . rooney alianza soka lake kwenye klabu ya everton na akiwa na umri wa  miaka 16 mkongwe david seaman alipata joto ya jiwe baada ya kushuhudia shuti la rooney likiishia kwenye wavu wake na kuinyima arsenal rekodi ya kutofungwa kwenye mechi 30 . akiwa na miaka kumi na nane rooney alisajiliwa na manchester united na mechi yake ya kwanza ilikuwa kwenye ligi ya mabingwa dhidi ya fernabace . rooney alifunga mabao matatu siku hiyo na kumdhihirishia kila mmoja kuwa sir alex ferguson alikuwa anajua anachofanya alipopambana kumsainisha.

kabla ya mabao matatu ya juzi zakaria bakali aliitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya ubelgiji , watu wengi walishtushwa na kitendo cha kocha marc wilmots kumuita mtu ambaye anaweza kuwa sehemu ya kikosi cha under 17 kwenye timu iliyojaa wachezaji wakubwa kama kina edin hazard na kevin mirallas .
baada ya mchezo wa juzi kila mmoja amekiona kile kilichoonwa na marc wilmots , huyo ndio zakaria bakalli.
 

No comments:

Post a Comment