Thursday, August 29, 2013

UKATILI GANI HUU



Polisi nchini Uchina imetangaza kuwa itatoa zawadi kwa yeyote atakayetoa habari zitakazowasaidia kumkamata mama mmoja ambaye anashukiwa kumng'oa macho mvulana mwenye umri wa miaka sita.
Shambulio hilo linasemekana kutokea tarehe ishirini na nne mwezi huu katika eneo na Fenxi, iliyoko katika mkoa wa Shanxi.
Mvulana huyo anasemekana alikwenda kucheza na watoto wengine lakini wazazi wake walimpata baadaye huku macho yake yote yakiwa yamengolewa huku akivuja damu.
Mvulana huyo kwa sasa anaendelea kupata matibabu hospitalini.
Idara ya polisi nchini humo imetoa zawadi ya zaidi ya dola elfu kumi na sita kwa yeyote atakayetoa habari, kuhusu aliyehusika na shambulio hilo.
Wazazi wa mtoto huyo wanasemekana kuwa wakulima.
Mamake amesema mtoto huyo aliwaambia kuwa wakati alipokuwa akitembea alishambuliwa na mama mmoja ambaye hakumfahamu.
Polisi walipata macho ya mvulana huyo karibu na eneo la tuko.
Uchunguz wa awali umebainisha kuwa sehemu ya mboni au Cornea kwa Kiingereza ilikuwa imengolewa, na hivyo kuashiria ulanguzi wa viungo vya kinadamu.
Hata hivyo polisi wanasema hawajatambua chanzo cha shambulio hilo.

BBC Swahili

No comments:

Post a Comment