Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA), Profesa John Nkoma akizungumza na wadau mbali mbali wa maswala ya
habari hapa nchini wakiwemo wamililiki wa magazeti tando (Blogggers) juu ya
kampeni mpya ya kuhamasisha matumizi mazuri ya Mitandao ya Mawasiliano hapa
nchini, leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania, Uliopo eneo la Sinza B,jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA), Innocent Mungy
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA), Profesa John Nkoma akifafanua jambo zaidi.
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA), Innocent Mungy akifafanua jambo wakati wa Warsha ya siku moja kwa wadau
mbali mbali wa maswala ya habari hapa nchini wakiwemo wamililiki wa magazeti
tando (Blogggers) juu ya kampeni mpya ya kuhamasisha matumizi mazuri ya
Mitandao ya Mawasiliano ,iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao
Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Uliopo eneo la Sinza B,jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA), Profesa John Nkoma akibonyeza kitufe kwenye Kompyuta ikiwa ni ishara ya
uzinduzi wa Wimbo wa kampeni mpya ya kuhamasisha matumizi mazuri ya Mitandao ya
Mawasiliano hapa nchini.
Baadhi ya Washiriki wa
Warsha hiyo kwa wadau mbali mbali wa maswala ya habari hapa nchini wakiwemo
wamililiki wa magazeti tando (Blogggers) juu ya kampeni mpya ya kuhamasisha
matumizi mazuri ya Mitandao ya Mawasiliano ,iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa
Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Uliopo eneo la Sinza
B,jijini Dar es Salaam
Msanii wa Muziki wa Kiasili,Mrisho Mpoto akisisitiza
jambo juu ya umuhimu wa Mawasiliano Mazuri ya Mitandao wakati wa Warsha ya siku
moja kwa wadau mbali mbali wa maswala ya habari hapa nchini wakiwemo wamililiki
wa magazeti tando (Blogggers) juu ya kampeni mpya ya kuhamasisha matumizi
mazuri ya Mitandao ya Mawasiliano ,iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano
wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Uliopo eneo la Sinza B,jijini
Dar es Salaam.
Mmoja wa Wamiliki wa Magazeti tando hapa nchini (Blogger),
John Bukuku kutoka Full Shangwe Blog akitoa shukrani zake za dhati kwa TCRA
ikiwa ni kwa niaba ya Bloggers Wengine baada ya kutambuliwa kuwa ni sehemu ya
vyombo ya Habari hapa nchini.
KAMPENI YA KUHAMASISHA MATUMIZI MAZURI YA MAWASILIANO
Siku za hivi karibuni, ongezeko la huduma za mawasiliano
nchini limekuwa kwa kasi sana. Huduma za mawasiliano nchini katika kipindi
kifupi zimekuwa sana na kuwafikia Watanzania wengi zaidi. Kutoka laini za simu
za mkononi milioni tatu tu mwaka 2000
hadi kufikia laini 28,000,000.
Watanzania walio wengi hivi sasa wanafaidika kwa huduma
za mawasiliano, yakiwemo mawasiliano ya simu za mikononi, utangazaji. Vile vile
huduma za ziada kama kutuma na kupokea fedha kwa kutumia mitandao na simu za
mkononi zimeongezeka maradufu. Wananchi wengi wanapata huduma za kibenki kwa
kutumia simu zao, wanawasiliana kwa kutumia simu zao kupitia sauti, SMS na
kadhalika.
Hali kadhalika kumekuwa na ongezeko la matumizi ya
intaneti kwa watanzania walio wengi kutoka watumiaji laki tatu miaka mitatu
iliyopita hadi watumiaji milioni 7.6 kwa takwimu za hivi karibuni. Wengi wa
watumiaji wa intaneti matumizi yao ni katika kujifunza na kujielimisha pamoja
na matumizi ya mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, BBM, LinkedIn
na blog mbalimbali zinazotoa habari mbalimbali zikiwemo za kimaendeleo,
burudani pamoja na michezo.
Matumizi haya ya intaneti yamewanufaisha watanzaia walio
wengi kwani ni fursa murua ya kujifunza kupitia mitandao hiyo ya kijamii kwa
kupata habari mpya, kujifunza na kuelimishana kuhusu shughuli za maendeleo na
kuleta amani miongoni mwa watanzania.
Hata hivyo pamoja na maendeleo haya, kumekuwepo na baadhi
ya watu wachache wanaotumia mawasiliano ya simu, mitandao ya kijamii, redio, TV
na mawasiliano mengine kwa lengo la kuvuruga amani, kuchocheo vurugu,
kuchonganisha watu, kusababisha ugomvi, kuwaumiza wengine kwa mambo yasiyo na
ukweli, kupotosha jamii na hata kuvuruga maendeleo kwa ujumla.
Leo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inazindua
kampeni ya kuelimisha umma kuhusu matumizi mazuri ya mawasiliano na
inawatahadharisha wananchi kwamba kutumia mawasiliano vibaya kama
ilivyoainishwa katika sheria ya Mawasiliano ya Kielectroniki na Posta (EPOCA)
ya mwaka 2010 ni makosa. Katika kampeni hii, Mamlaka inakusudia kuwasihi
wananchi kuhakikisha wanatumia mawasiliano vizuri ili kudumisha amani,
mshikamano na upendo miongoni mwa watanzania.
Katika uzinduzi huu, Mamlaka imewaalika baadhi ya
watumiaji mahiri wa mitandao ya kijamii ambao wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha
watanzania walio wengi wanafaidika na mawasiliano. Miongoni mwao wako wamiliki
wa blog mbalimbali, wasimamizi wa makundi mbalimbali katika mtandao wa FB na
mengineyo. Nia ya Mamlaka ni kuomba ushirikiano kwao ili waweze kushiriki
katika kampeni hii na kuwahamasisha mashabiki wao kutumia vizuri mitandao ya
kijamii ili kunufaisha Taifa letu kwa matumizi mazuri.
Watumiaji wa simu za mkononi na wananchi wote
wanashauriwa kuunga mkono juhudi zinazofanyika ili kufanikisha kampeni hii kwa
ajili ya kudumisha na kuendeleza amani na usalama na kuharakisha maendeleo ya
sekta ya Mawasiliano inaendelea kuchangia uchumi wa Taifa na kuiweka Tanzania
katika mazingira mazuri zaidi kijamii, kiuchumi na kisiasa.
Tunawasihi wananchi na watumiaji wa huduma za mawasiliano
kuwa wakipokea ujumbe wowote wa kueneza chuki, unaopelekea kuvuruga amani,
uchochezi na kuvuruga amani, toa taarifa kwa vyombo husika, kisha futa ujumbe
huo. Usiueneze kwa wengine kwani utakuwa sehemu ya uhalifu.
Imetolewa na:
MKURUGENZI MKUU
Mamlaka ya mawasiliano TaNzania
31 Julai 2013
No comments:
Post a Comment