Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia alipofungua
Mkutano wa kwanza wa Kimataifa wa Kutangaza Utalii kwa Nchi za Bara
la Afrika na Kuhamasisha Utalii Endelevu katika nchi hizo.
Mkutano huo umefunguliwa leo Oktoba
15, 2012 katika Ukumbi wa AICC leo Oktoba 15 Jijini Arusha na kuhudhuriwa
na mawaziri 17 kutoka nchi mbalimbali za Afrika. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto) akipokea barua ya
wazi kutoka kwa Katibu wa Mkuu wa Shirika la Utalii la Dunia, Taleb Rifai,
iliyotolewa na Baraza la Waendesha Utalii Duniani (WTTC) mara baada ya
kufungua Mkutano wa Kuhamasisha utalii barani Afrika leo, Oktoba 15, 2012,
jijini Arusha. Katika Mkutano huo pia umehudhuriwa na Mawaziri 17 kutoka
nchi mbalimbali za Afrika.Picha na OMR
Makabidhiano yamekamilika
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akipunga mkono kuwaaga wasanii wa ngoma ya asili wa kabila la kimasai
wakati akiondoka katika ukumbi wa mikutano wa AICC jijini Arusha leo Oktoba 15,
2012 baada ya kufungua mkutano wa kwanza wa Kimataifa wa Kutangaza Utalii
kwa Nchi za Bara la Afrika na Kuhamasisha Utalii Endelevu katika nchi
hizo.Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia Pakti ya kifuko
cha unga wa Ubuyu na kusikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Masoko na Mauzo
wa kampuni ya Moringa Consultancy (TZ) Co Ltd, Christina Ngoti, wakati
Makamu alipokuwa akitembelea Mabanda ya Maonyesho baada ya kufungua mkutano wa
kwanza wa Kimataifa wa Kutangaza Utalii kwa Nchi za Bara la Afrika
na Kuhamasisha Utalii Endelevu katika nchi hizo. Mkutano huo umefanyika
leo
Oktoba 15, 2012 jijini Arusha. Picha
na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka
kwa Mtaalam wa Tiba za Asili, James Kangaa, wakati Makamu alipokuwa
akitembelea Mabanda ya Maonyesho baada ya kufungua mkutano wa kwanza wa Kimataifa wa Kutangaza Utalii
kwa Nchi za Bara la Afrika na Kuhamasisha Utalii Endelevu katika nchi
hizo. Mkutano huo umefanyika leo Oktoba 15, 2012 jijini Arusha. Picha na
OMR
No comments:
Post a Comment