Friday, October 19, 2012

RAIS KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI KUZINDUA UJENZI WA JENGO LA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI OMAN


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi kuashiria kuanza rasmi ujenzi wa jengo la ubalozi wa Tanzania  nchini Oman katika mtaa wa balozi jijini Muscat Oman .Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe, (watatu kushoto) ni Balozi wa Tanzania nchini Oman, Ali Ahmed Saleh na (kulia) ni Afisa Mwandamizi Ubalozi wa Tanzania nchini Oman,  Bwana Abdallah Kilima.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizindua ujenzi wa jengo la ubalozi wa Tanzania nchini Oman .Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe,watatu kushoto ni  Balozi wa Tanzania nchini Oman, Bw. Ali Ahmed Saleh, (wanne kulia aliyeshika karai) ni Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Oman, Bw. Abdallah Kilima na (kulia anayeshuhudia) ni  Afisa katika Ubalozi huo, Bw. Saidi Mussa.

No comments:

Post a Comment