Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua
rasmi Mkutano Mkuu wa mwaka wa Viongozi wa Takukuru, uliofanyika katika Ukumbi
wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 17, 2012. Mkutano huo
unatarajiwa kumalizika kesho.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Waziri wa
Katiba na Sheria, Mathias Chikawe.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Edward Hosea, nje ya Ukumbi
wa Mlimani City, mara baada ya kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa mwaka wa Viongozi
wa Takukuru.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa
Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Edward Hosea, mara baada ya kufungua rasmi Mkutano
Mkuu wa mwaka wa Viongozi wa Takukuru.
No comments:
Post a Comment