WAANDAJI wa mbio za Rock City Marathon 2012 wametangaza kusogeza mbele usajili wa kushiriki mbio hizo mpaka Oktoba 26 ili kutoa fursa kwa watu wengi zaidi kushiriki katika mbio hizo. Akizungumza na waandishi jijini Dar es Salaam jana, mratibu wa mbio hizo toka kampuni ya Capital Plus International (CPI), alisema kuwa wameamua kusogeza mbele usajili kutokana na namba ya waombaji kuendelea kuongezeka ili kushiriki mbio za mwaka huu.
Bi
Sanga alisema tukio hilo linaloandaliwa na kampuni ya Capital Plus
International (CPI) na kudhaminiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Taifa ya Jamii
(NSSF), Airtel Tanzania, Geita Gold Mine, Shirika la Ndege la Air Tanzania,
Parastal Pension Fund (PPF), African Barrick Gold, New Africa Hotel, Nyanza
Bottles, New Mwanza Hotel, TANAPA na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) limewavutia
washiriki wengi kutoka nchi mbalimbali ambao wasingependa kukosa mbio hizo
mwaka huu. “Tumekuwa tukipokea simu kutoka kwa washiriki mbalimbali, kutoka
Chama cha Riadha nchini na kutoka nchi jirani ambao wanataka kupewa nafasi ya
kushiriki katika mbio za mwaka huu. Sisi kama waandaji tumeona ni vyema
tuwapatia nafasi ya kujisajili kwa kuwa ushiriki wa utasadia lengo la mbio za
mwaka huu lifikiwe la kutangaza utalii kupitia michezo,” alisema Sanga.
Bi
Sanga aliongeza kuwa washiriki na washabiki wa mbio za Rock City za mwaka huu
watapata fursa ya kumshuhudia msanii maarufu wa Tanzania Juma Nature a.k.a Sir
Nature na kundi lake la TMK Wanaume wakitumbuiza wakati wa mbio hizo.
Alisema kuwa washiriki kutoka nchi tisa wameshathibitisha
kushiriki mbio za kilometa 21 za mwaka huu zitakazofanyika katika uwanja wa CCM
Kirumba jijini Mwaka tarehe 28 mwezi Oktoba.
Bi
Sanga alisema kuwa mialiko katika mbio hizo imeongezwa na wanariadha kutoka Afrika
Mashariki na nchi nyingine za ulaya wanatarajiwa kushiriki. Akilitaja nchi hizo
kuwa ni Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Demokrasia ya Watu wa Kongo (DRC) na
nchi nyingine za ulaya kama Australia, India, Canada na Marekani.Alisema kuwa
wanauhakika mkubwa kuwa namba ya washiriki mwaka huu itaongezeka mara dufu
kutokana na uboreshwaji wa zawadi.
“Tunatarajia
kuwa na washiriki wengi zaidi toka nchi za nje ukilinganisha na miaka
iliyopita. Hii inaonyesha kukua mbio hizi na kuwa ushindani wa mbio za mwaka
utakuwa mkali zaidi,” alisema Bi Sanga.Mbio hizo za kila mwaka zimegawanyishwa
katika makundi matano, ambapo kutakuwa na mbio za kilomita 21 kwa wanawake na
wanaume, kilomita tano kwa watu wote, kilomita tatu kwa watu wenye ulemavu,
kilomita tatu kwa wazee (miaka 55 na kuendelea) na kilomita mbili kwa watoto
umri kati ya miaka saba mpaka kumi.
Bi.
Sanga alisema kuwa mbio hizo zinazoonyesha mafanikio makubwa toka zizinduliwe
mwaka 2009, zinalenga kukuza utalii wa ndani kupitia michezo kama kauli mbiu
yake inavyosema ‘tukuze utalii wa ndani kupitia michezo’. “Jiji la
Mwanza ni tajiri sana katika vivutio vya utalii na tumelenga kumpitia mbio hizi
kuvitangaza vivutio hivyo. Mbio za kilomita 21 zitaanza katika uwanja wa CCM
Kirumba na kupita njia tofauti tofauti na kurudi CCM Kirumba”,
Alisema
pia pesa itakayopatikana ikitokana na ada ya usajili toka kwa washiriki moja
kwa moja itapelekwa katika mfuko wa msaada kwa watu wenye ulemavu waishio
jijini Mwanza. Fomu za usajili za mbio hizo zinapatikana katika
uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza, Ofisi za Kampuni ya Capital Plus
International Ltd zilizopo jengo la ATC ghorofa ya tatu, na pia zinapatikana
katika blog ya rockcitymarathon.blogspot.c
No comments:
Post a Comment